Uswahiba kati ya wasanii wawili wa Bongo Flava nchini, Afande Sele na 20
Percent umeingia dosari baada ya kutupiana maneno kila mmoja kwa
nyakati tofauti kwenye vyombo vya habari.
Maneno hayo yalianza wiki iliyopita baada ya Afande Sele kuzungumza na
Clouds FM na kudai kusikitishwa na kitendo cha swahiba wake 20 Percent
cha kugoma kutumbuiza kwenye tuzo za muziki za Zanzibar wakati alikuwa
amelipwa pesa zote.
Kufuatia mgomo huo, waandaaji walimpeleka lock-up msanii huyo na kubaki
na laptop yake mpaka pale atakapowarudishia waandaji hao shilingi
milioni moja waliyompa kwaajili ya kuperform kwenye tuzo hizo.
Hatimaye jana 20 Percent alizungumza na kituo hicho cha radio kuhusiana
na tukio lenyewe na kusema kuwa Afande Sele amechanganyikiwa na
anasumbuliwa na njaa ndio maana anamlaumu.
Akiongea kwa jaziba, 20 Percent amesema Afande Sele ni kama ‘mtoto’ na
alimshangaa kufahamu kuwa alifika Zanzibar saa sita usiku bila kuwa
sehemu ya kulala kutokana na waandaaji hao kuwa wababaishaji.
Amesema waandaji wa tuzo hizo ni ‘wahuni’ tu ndo maana alikataa
kuperform na kuongeza kuwa maisha yake hayategemei muziki wa Bongo
Flava.
Kuhusu Laptop yake iliyobaki kwenye mikono ya waandaji wa tuzo hizo,
msanii huyo wa ‘Tamaa Mbaya’ amesema hatoifuata Zanzibar bali
watampelekea wenyewe.
Miaka ya hivi karibuni, Afande Selena 20 Percent walionekana kuwa
maswahiba wa nguvu lakini tukio hilo linaonesha kuutulia doa ushkaji
wao. |
No comments:
Post a Comment