Mshambuliaji wa kimataifa
wa Simba na Zambia Felix Muamba Sunzu leo amerudi dimbani kuitumikia tena klabu
yake ya Simba na kuifungia goli la pekee na la ushindi kwenye mchezo wa kombe la
Urafiki linaloshindaniwa huko Zanzibar.
Simba imeifunga timu ya
vijana ya Zanzibar Karume Boys kwa bao 1-0 liliowekwa kimiani na Mzambia
huyo.
Kwa matokeo hayo
Simba ambao walianza vyema michuano hiyo inayofanyika kwenye Uwanja wa
Amaan mjini hapa kwa ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya mabingwa wa Zanzibar,
Mafunzo kabla ya kuja kushikiliwa kwa sare ya 1-1 na Azam, ambao ni washindi wa
pili wa Ligi Kuu ya Bara.
Azam FC ilimaliza ikiwa ya pili
kwa kuwa na pointi 5 baada ya sare mbili na ushindi katika mechi iliyochezwa
mapema jana.
Katika
mechi hiyo, Azam iliilaza Mafunzo ya hapa kwa mabao 3-2.
|
No comments:
Post a Comment