Saturday, July 7, 2012

SABABU YA TIMU YA COPA COCACOLA IRINGA KUTOLEWA YATAJWA NA IRFA

Chama cha soka mkoa wa Iringa ( IRFA) kimeeleza sababu ya timu ya vijana wa mkoa wa Iringa iliyoshiriki Copa Cocacola kutolewa mapema katika mashindano hayo kuwa ni kutokana na mwamko mdogo wa wakazi wa mkoa wa Iringa .

Katibu mtendaji wa IRFA Eliud Mvella Wamahanji ametoa kauli hiyo Leo katika ukumbi wa VETA mjini Iringa wakati wa kumpongeza aliyekuwa katibu mkuu wa shirikisho ya mpira wa miguu nchini ( TFF) Frederick Mwakalebela ambaye amejitolea kuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya wilaya ya FA wilaya (Mwakalebela Cup 2012)

Wamahanji alisema kuwa mbali ya Mwakalebela kujitolea kuwa mdhamini katika mashindano hayo ila ndie aliyejitolea awali kusaidia jezi timu hiyo ya Copa Cocacola ila zaidi yake hakuna hata mdau mmoja ambaye amejitolea kusaidia timu hiyo.

Aidha Wamahanji alisema kuwa pamoja na jitihada mbali mbali ambazo IRFA imekuwa ikizifanya katika mkoa wa Iringa kuendeleza michezo ila bado wapo baadhi ya watu ambao ni wakazi wa mkoa wa Iringa wamekuwa ni mabingwa wa kusemamea vibaya mkoa badala ya kusaidia .

Hata hivyo alionya tabia ya baadhi ya watu mkoa wa Iringa kuendesha mashindano kinyume na taratibu na kanuni za soka kwa kuchezesha mashindano bila haraka za TFF .

Awali mwenyekiti wa Chama cha soka Manispaa ya Iringa ( IMFA) Ramadhan Mhano alitaja timu ,ambazo zitashiriki katika mashindano hayo FA Mwakalebela Cup ni pamoja na Mkwawa FC, Lipuli FC, BBC FC, Real moja FC ,Don Bosco FC, Magereza FC ,Mlandege FC, Ruaha FC,Uhuru FC, Sengo FC,Nyota Njema FC, Mshindo FC,Young stars FC na Upendo FC.

No comments:

Post a Comment