Thursday, July 26, 2012

Aliyetangaza Kujinyonga Kwa Kiingilio Amehairisha Kutekeleza Zoezi Hilo

Katika mazingira ya kutatanisha aliyewahi kuwa mfanyabiashara maarufu mkoani Iringa Bwana Makosa alitangaza kujinyonga katika tukio ambalo alidai atalifanya hadharani na atayetaka kushuhudia atalipia kiingilio ambacho kwa mujibu wake kingesaidia familia yake na watoto yatima. Mjengwa Blog ilimtafuta ili kujua kwanini ameamua kufanya hivyo na afikirii kama kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria za jamhuri na hata katika vitabu vya dini jambo hilo ni dhambi kubwa maana mwenye mamlaka juu ya kuchukua uhai wa mtu ni yule aliyetoa uhai ambaye sote tunaamini ni Mungu mmoja aliye juu mbinguni, Sasa kwanini Makosa ameamua kufanya hivi? ifuatayo ni Execlusive Interview fupi kati ya mdau wa Mjengwa Blog Na Makosa ambayo ilibidi ifanyike baa maana sikuwa na Miadi naye kwahiyo ilikuwa ni ghafla tu
Mdau:Je ni lini unatarajia kutimiza lengo lako la kutaka kijinyonga?
Makosa: Embu nichukulie kiroba kwanza
Mdau: Kwahiyo nikikununulia kiroba kitakuwa ndio kiingilio changu siku ambayo utajinyonga?
Makosa:Sijinyongiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Mdau: Kwahiyo umehairisha zoezi la kujinyonga ?
Makosa:Sijinyongiiiiiii
Baada ya hapo makosa akaanza kinipa Free style yaani alikuwa ananiimbia nyimbo aliyoniambia anataka kwenda kuirekodi hivyo akaniomba ushauri ni studio gani anaweza kwenda.
Mdau: Nadhani kwa jinsi unavyoimba ukienda kwa Marco Chali ataitendea haki nyimbo yako
Nikamwambia kama anaweza kuimba kidogo labda naweza kuwa meneja wake nikivutiwa na kipaji chake
Pata ladha ya mistari ya wimbo wa Makosa
Makosa: "Watoto wangu wana miiili midogo dogo ila wana Sauti" KUBWAAA, mke wangu anamwili mdogo mdogo mdogo ila ana mat*** MAKUBWAA, Toka siku nyingi mimi marafiki zangu ni watu "WAKUBWAA,
Mdau: Inatosha inatosha nimekubali kweli we ni mtu mkubwaaa ha ha ha ha
Wadau wa blog hii hiyo ilikuwa execlusive interview kati yangu na Jamaa aliyetangaza kujinyonga kwa kiingilio je mdau unaweza kumuweka katika kundi gani?

No comments:

Post a Comment