Mwanahabari maarufu ambaye pia ni mwandishi wa Blogi amefungwa
jela miaka 18 nchini Ethiopia kwa madai ya kukiuka sheria ya ugaidi.
Eskinder Nega na wenzake 23 walipatikana na hatia mwezi uliopita.
Walikamatwa kwa madai ya kuwa na uhusiano na kundi moja la upinzani lililo na
makao yake Marekani kwa jina Ginbot Seven.
Serikali ya Ethiopia inadai kuwa kundi hilo ni la kigaidi.
Mahakama hiyo ya Addis Ababa pia ilimfunga jela maisha mwanaharakati wa
upinzani,Andualem Arage.
Kutokana na kazi yake ya uwana-habari na kuandika Blogi, Mwezi wa May,
Eskinder alipewa tuzo maarufu la kimarekani la Pen America's Freedom to
Write.
Makundi ya kutetea haki za kibinadamu zimekuwa ikiilaumu serikali kwa kubuni
sheria hiyo ya kukabiliana na ugaidi yakisema sheria hiyo haifai.
Siku ya Ijumaa Mwanahabari ,Eskinder na mwanachama wa chama cha upinzani cha
Unity for Democracy and Justice party walikuwa mahakamani kuhukumiwa.
Washukiwa wengine 16 waliopatikana na hatia mwezi wa Juni wako
ukimbizini.
Walipokuwa wakiingia mahakamani wawili hao waliwapungia mikono jamaa zao na
marafiki pamoja na maafisa wa kibalozi waliokuwemo ndani.
Eskinder alikamatwa mwezi wa Septemba mwaka jana baada ya kuandika makala
iliyokuwa ikiilaumu serikali ya Ethiopia kwa kukamata wapinzani wake kwa kutumia
sheria ya ugaidi.
Miongoni mwa watu ambao wamekamatwa chini ya sheria hiyo ni msanii na mcheza
filamu maarufu nchini Ethiopia, Debebe Eshetu ambaye ni mkosoaji mkuu wa
serikali.
|
No comments:
Post a Comment