Tuesday, August 28, 2012

MDAU NA NYAMA ZA RUAHA MBUYUNI- ZIMENONA!!


Ni eneo la Ruahambuyuni, ndizi choma na nyama zake kwa bei poa, hiyo ni kutokana na eneo hilo kufugwa sana wanyama wadogo wadogo kama Mbuzi.


"Chagua ile pale ndiyo nzuri", ni mdau naye akitoa ushauri wa kupata nyama na ndizi nzuri.

Wakamatwa Mombasa sababu ya Rogo

Watu 12 wamekamatwa na polisi kufuatia makabiliano kati ya polisi na vijana wanaofanya vurugu kufuatia kuuwawa kwa kiongozi wa kidini Sheikh Aboud Rogo siku ya jumatatu.Katika siku ya pili ya vurugu hizo, wengi ya vijana hao wamekamatwa nje ya Msikiti Musa iliyo eneo la Majengo visiwani Mombasa.
Wakati wa makabiliano hayo polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa na ghadhabu.Hata hivyo katika eneo moja polisi walilazimika kutumia risasi za mpira kuwatawanya vijana waliokuwa wakiwasha matairi barabarini na kufanya uporaji.Bwana mmoja alichomwa kisu katika karakana yake na kulazimika kupewa huduma ya kwanza na wafuasi wa dhehebu la Jeshi la wokovu.Na wakati Mombasa ikiwaka moto, wapiganaji wa Al shabaab wametuma ujumbe katika mtandao wao wakiwasihi waislamu wa kenya "wachukuwe kila hatua zinazostahili kulinda dini yao"" Waislamu lazima wachukue sheria mikononi mwao, na wasimame kidete dhidi ya makafiri na kuchukua kila hatua kuilinda dini yao, heshima yao ,mali yao na maisha yao kutoka kwa maadui wa waislamu" , Al shabaab wamenukuliwa wakisema hayo katika taarifa yao.Kiongozi huyo wa kidini Sheikh Aboud Rogo ,aliyepigwa risasi na kuuwa siku ya jumatatu alikuwa ametajwa na Marekani pamoja na Umoja wa Mataifa kama mtua anayewasajili baadhi ya vijana wa Kenya wkenda kujiunga na wapiganaji wa Al Shabaab.Sheikh Aboud Rogo pia anadaiwa kuwa alikuwa mfadhili wa kundi hilo la Al shabaab.

MTOTO AFANYA MAPENZI NA MAMA YAKE KWA MIAKA 10, WENYEWE WAISHI KAMA MKE NA MUME


Mwandishi wetu, Ruvuma Yetu
Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maendelo ya Jamii, Jinsia na watoto kuingilia kama kuna sheria inayomruhusu Mtoto na Mama yake mzazi kuweza kuishi kindoa.
Hayo yamebainika katika Kijiji cha Namabengo Wilaya ya Namtumbo baada ya Joseph Mapunda kuweza kuishi na Mama yake kindoa kwa miaka 10 mfululizo.
Joseph Mapunda amesema ameweza kuishi kindoa na Mama yake Mzazi baada ya yeye kukubaliana wenyewe yeye na mama yake mzazi kuishi kindoa kama mke na mume.
Alipoulizwa mama anayefahamika kwa jina la Kondrada Ngonyanialikiri kuwa kweli wameishi kindoa kwa miaka 10 na anampenda Mume wake ambaye ni Mtoto wake Joseph Mapunda.
Umati wa watu uliofurika kwa Mganga wa Jadi Flora Ndembo, Namabengo wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma watu wapatao 400 wameomba Serikali ichukue mkondo wa Sheria kuvunja ndoa hiyo.
Kwa Mkoa wa Ruvuma hii ni mara ya kwanza mtoto wa kiume kutembea na mama yake mzazi.
Blogzamikoa

Friday, August 24, 2012

KWANZA JAMII IRINGA LIPO MTAANI WIKI HII NA HABARI MOTOMOTO!



Uingereza yaibembeleza Ecuador

Uingereza imeandika barua kwa ubalozi wa Ecuador mjini London ikitaka kurejelea mazungumzo kuhusu hatma ya Julian Assange, mwanzilishi wa mtandao wa kufichua siri wa Wikileaks, aliyetorokea katika majengo ya ubalozi huo kuepuka kurejeshwa nchini Sweden kwa lazima.
 
Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ulivurugika baada ya uamuzi wa Ecuador kumpa bwana Assange hifadhi ya kisiasa na Uingereza kutishia kuvamia ubalozi huo na kumkamata.
 
Afisi inayoshughulika na masuala ya kigeni haijasema chochote kuhusu ujumbe uliokop kwenye barua hiyo lakini afisa mmoja ameelezea kuwa inanuia kutuliza hali kati ya mataifa hayo mawili.
Rais Rafael Correa ameiambia BBC kuwa Uingereza ilifanya makosa makubwa kwa kutishia kuingia kwa nguvu kwenye ubalozi wa Equador,''Huu ni mvutano ambao ungeisha iwapo Uingereza ingetoa hakikisho ya kupita kwa usalama kwa Bwana Assange au unaweza kuendelea kwa miezi na hata miaka iwapo hataweza kutoka kwenye ubalozi wetu hapa London kuelekea Equador.''
Huenda mataifa ya Amerika Kusini yakamuunga mkono rais Rafael Correa.
Huku Uingereza ikisema kuwa inataka kurejelea mashauriano kuhusu hatma ya Julian Assange, Equador haikubaliani na msimamo huo na inataka kuhakikishiwa kuwa Assange hatakamatwa iwapo atatolewa kwenye ubalozi wao nchini Uingereza kuelekea Equador.
Equador inataka pia kuhakikishiwa kuwa mwanzilishi huyo wa mtandao wa Wiki Leaks hatawahi kupelekwa Marekani anakokabiliwa na tuhuma za kutoa taarifa muhimu na za siri kwenye mtandao wake.
Hata hivyo hakuna matumaini kwamba Marekani itakubali hilo.
Kwa hiyo ubalozi wa Equador umekiri kuwa huenda ukampa bwana Assange hifadhi kwa miaka mingi.
 


Tuesday, August 14, 2012

VYUNGU VYA LUNGEMBA NI UTALII ULIOTEREKEZWA

 


Wateja wakiangalia vyungu vya kupikia na mapambo ya ndani na nje ya nyumba, yaliyotengenezwa kwa udongo, katika kijiji cha Lungemba katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Mteja akichagua moja ya chungu kwa ajili ya shughuli zake nyumbani, kila sanaa ina bei yake kulingana na ukubwa, urembo na ubunifu.

Mfinyanzi akisubiri wateja, kama alivyokutwa, wafinyanzi hao wamekuwa wakitengeneza vitu mbalimbali kwa kutumia udongo mfinyanzi na hivyo kujitengenezea ajira kutokana na kazi hiyo kuwainggizia kipato.

Mfinyanzi wa sanaa hizo za udongo akimuonyesha mteja moja ya kazi yake ya mikono, ambayo huitengeneza kwa udongo.



Helikopta za kivita za Uganda zapatikana

Jeshi la Uganda limesema kuwa helikopta zake nne zilizokuwa zime ripotiwa kutoweka zikiwa njiani kuelekea nchini Somalia sasa zimepatikana na marubani wake wote wako salama.
Akizungumza na BBC msemaji wa jeshi hilo Kanali Felix Kulaigye hakuweza kusema ndege hizo ziko wapi kwa sasa.
Naye msemaji wa jeshi la Kenya, Bogita Ongeri ameiambia BBC kwamba operesheni ya kutafuta ndege hizo ilikuwa imevurugwa na hali mbaya ya hewa na kuongeza kuwa helikopta hizo nne zilikuwa kwenye safari hiyo kutoka nchini Uganda.
Moja ya helikopta hizo ilitua katika mji wa Garissa.
Rubani aliyekuwa kwenye helikopta ya pili alizungumza na mamlaka za kenya akisema yuko katika eneo la mlima kenya lakini hakukukuwa na mawasiliano na helikopta nyingine mbili.
Helikopta hizo za Uganda hutumiwa kusindikiza misafara kutoka angani, katika opereresheni za utafutaji na uokoaji pamoja na kushambulia wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabaab nchini Somalia.
Helikpta hizo ni miongoni mwa ndege ambazo zilikuwa zikielekea Somalia kukipa nguvu kikosi cha Umoja wa Afrika .
Awali msemaji wa jeshi la Uganda Kanali Felix Kulayigye alikuwa amesema kuwa walikuwa wakizitafuta ndege zao mbili aina ya Mi-24 . Alisema ndege hizo ni zile za kufanya mashambulizi.

Friday, August 10, 2012

Rudisha arudisha fahari ya Kenya

Mkenya David Lekuta Rudisha ameibuka kuwa mwanariadha wa kwanza kuandikisha rekodi mpya kwenye mashindano ya riadha katika michezo ya Olimpiki, inayoendelea jijini London Uingereza na kisha kushinda medali ya dhahabu katika mbio za mita mia mbili.
Akiwa anashiriki fainali ya michezo ya Olimpiki kwa mara kwanza, Rudisha mwenye umri wa miaka 23 alinyakuwa ushindi huo kwa kuwa mtu wa kwanza kukimbia umbali wa mita mia nane kunako dakika 1, sekunde 40 nukta 91.
Mwariadha wa Botswana Nijel Amos, umri 18, alinyakuwa medali ya fedha huku chipukizi mwingine kutoka Kenya Timothy Kitum, akiridhika na medali ya shaba.
Mwingireza Andrew Osagie alimaliza katika nafasi ya nane lakini akaweza kuandikisha muda bora wa dakika 1:43.77.
Rudisha ambaye ni bingwa wa dunia aliongoza katika mbio hizo tangu mwanzo hadi mwisho na kuwaacha wanariadha wenzake kwa tofauti ya sekunde 49.28. Kisha akafyatuka katika hatua za mwisho mwisho na kuivunja rekodi yake mwenyewe.
Huku kila mwanariadha akiwa na msukumo wa kasi ya rudisha, ni Abubakar Kaki wa Sudan tu ndiye aliyeshindwa kuandikisha muda wake bora licha ya kukamilisha mbio hizo katika nafasi ya saba.
Rudisha ameiambia BBC: "Lo! Nimefurahi sana. Huu ni wakati ambao nimekuwa nikisubiri kwa kipindi kirefu. Kuja hapa na kuivunja rekodi ya dunia ni kitu ambacho bado sijaamini.''
" Nilikuwa nimejiandaa na sikuwa na shaka kwamba nitashinda. Leo, hali ya anga ilikuwa nzuri na niliamua tu kuparamia taji hili."
Ushindi wa Rudisha bila shaka ni habari njema kwa Kenya ambayo kinyume na matarajio, ilikuwa imeandikisha matokeo duni katika michezo hiyo ya Olimpiki kwa kuwa na medali moja pekee ya dhahabu.

Friday, August 3, 2012

Mwakyembe: Marufuku kuchimba dawa njiani!



Kama una mpango wa kusafiri kuelekea mikoani siku za hivi karibuni, jipange kupanda basi ukiwa umerekebisha haja ndogo mapema kabisaaa, kwakuwa utajuta mbeleni, hakuna kuchimba dawa tena, habari ndio hiyo!
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amepiga marufuku kuanzia sasa kwa mabasi ya abiria yaendayo mikoani kusimama eneo lolote njiani kwa madhumuni ya abiria kujisaidia haja ndogo maarufu sana kama ‘kuchimba dawa’.
Akizungumza wakati wa kutoa pendekezo la kuungwa mkono na wabunge kwa bajeti ya wizara yake, Mwakyembe alisema endapo basi litaonekana barabarani limepaki kwa ajili ya kuchimba dawa litafungiwa leseni.
Amesema jambo hilo humdhalilisha mwanamke ambaye amezaliwa na umbile la kujisitiri na pia hushusha heshima kwa wazazi.
Waziri huyo alisema abiria wote wanatakiwa kutumia nafasi hiyo kwenye vituo vikubwa wanavyosimama.
“Tutatoa onyo kwa mara ya kwanza,ya pili kama hatutajirekebisha basi tunachukua maamuzi[uamuzi] wa kumfungia leseni,kumuona mama yako anajisaidia ni sehemu ya kujilaani,hatuwezi kudhalilisha hivyo mama zetu,huo si utamaduni wetu” alisema Mwakyembe (Mwananchi).
Biashara ya juice njiani sasa imepata pigo!!!!

TAFAKARI YA LEO!..............

MGOMO WA WALIMU

Annan kujiuzulu wadhfa wake Syria



Mjumbe wa amani wa kimataifa nchini Syria, Kofi Annan, amesema kuwa mwenendo wa kutotaka kupatana kutoka kwa utawala wa rais Bashar al Assad ndiyo sababu kubwa ya hatua yake ya kujiuzulu ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.

Bwana Annan amesema kuwa harakati za kijeshi kutoka kwa wapiganaji wa upinzani pia zimechangia katika kufanya majukumu yake kuwa magumu na pia mgawanyiko uliokuwepo katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Miezi mitano iliyopita Kofi Annan alikabidhiwa jukumu Kubwa la kupatanisha utawala wa Rais wa Syria Bashar Al Assad na waasi wa upinzani wenye nia ya kumng'oa madarakani.

Lakini leo inaelekea maji yamezidi unga na Bw Annan ametangaza nia yake kujihuzulu.

Amesema hatua hiyo imechochewa na ukosefu wa Ushirikiano kutoka kwa Rais Assad na pia makundi ya waasi. Mpango wa kusitisha mashambulio uliopendekezwa na Bw Annan umekuwa ukipuuzwa na pande zote.

Serikali kwa upande wake imeendeleza mashambulio na kusababisha mauaji ya raia huku wapinzani nao wakiimarisha vita dhidi ya serikali.

Vilevile Bw Annan ameshtumu jamii ya kimatifa kwa kutounga mkono kikamilifu juhudi zake. Amesema huku umwagikaji damu ukiendelea nchini Syria jamii ya kimataifa imegawanyika kuhusu jinsi ya kutatua mzozo huo.

Rais Assad hajawahi kukubali upunzani kufanya maandamano ya kupinga utawala wake na badala yake amekuwa akitumia nguvu.

Amekuwa akiungwa mkono na Uchina na Urusi na hata kupewa msaada wa silaha.

Katika miezi ya hivi karibuni juhudi za Kofi Annan kutafutia mgogoro huo suluhu pia zimekuwa zikisambaratishwa na mgawanyiko kati ya baadhi nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Marekani,Uingereza na Ufaransa zimetofautiana vikali na Uchina na Urusi kuhusu mwelekeo unaofaa kumaliza mapigano nchini Syria.

Baada ya Kofi Annan kujihuzulu mwishoni mwa mwezi huu,haijulikani Umoja wa mataifa utakuwa na jukumu gani katika mpango wa kutafuta amani nchini Syria.

Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Susan Rice amesema juhudi za Annan hazingeweza kufaulu kutokana na utawala wa Rais Assad kupuuza mapendekezo ya kumaliza mapigano.

Naye Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema amejuta kujihuzu kwa Kofi Annan ambaye amemtaja kama mwanadiplomasia shupavu.

Serikali ya Syria inaendelea kutumia nguvu.

Hali katika mji mkuu Damascus ni ya kusikitisha na mjini Allepo makabiliano makali yanaendelea.

Mwelekeo wa Syria sasa umegeuka na kuwa vita badala ya amani.

CHANZO: BBCSWAHILI.COM

CWT IRINGA CHAONYA WANACHAMA WAKE ,CHAKOSOA HOTUBA YA RAIS DKT KIKWETE


Katibu wa CWT mkoa wa Iringa Bi.Veronica Mlungu

SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kulihotubia Taifa na kuzungumzia mgomo wa walimu unaoendelea ,chama cha walimu Tanzania (CWT) mkoa wa Iringa kimeibuka na kudai kuwa Rais Kikwete amepotoshwa juu ya madai ya walimu na kuwa wanachotaka walimu kuona haki ya misharaha kwa watumishi wote inazingatiwa si vinginevyo .

Huku kikiwaonya walimu walimu ambao ni wanachama wake kuwaCWT hakitakuwa tayari kuwasaidia walimu ambao wanaendelea na kazi iwapo wataharibu mali za shule ama kuwaadhibu wanafunzi na wazazi wakachukua hatua ya kuwafungulia mashtaka katika vyombo vya sheria.

Kauli hiyo imetolewa leo na katibu wa CWT mkoa wa Iringa Veronica Malungu alipozungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuhusiana na hotuba ya Rais Kikwete kwa Taifa juu ya mgomo huo wa walimu pamoja na malalamiko ya wazazi mkoani Iringa kwa badhi ya shule ambazo zimegoma huku walimu wake wakiendelea kuwacharaza fimbo na kuwapa adhabu kali wanafunzi.

Alisema kuwa CWT kama viongozi wa walimu hao iliwataka walimu wote kugoma na baada ya kugoma asiwepo mwalimu wa kwenda shule kufundisha hadi serikali itakaposikiliza kilio chao ,ila iwapo wapo walimu wanaokwenda shule na kuwaadhibu wanafunzi kama sehemu ya kulipiza hasira zao dhidi ya serikali kuwa hilo ni kosa na wakachukulia hatua hakutakuwa na utetezi wala msaada wowote toka CWT.

Kwani alisema kuwa makubaliano ya walimu wote ni kutofika kazini wala kukanyaga maeneo ya shule kujihusisha na wanafunzi hadi serikali itakapowasikiliza hivyo ni kinyume na makubaliano kuona baadhi ya walimu wachache wakikiuka makubaliano hayo na kuhamishia hasira zao kwa wanafunzi.

Pia alisema ni kosa kwa walimu ambao hawapo katika mgomo huo kuwatumikisha wanafunzi kazi za kufundisha wenzao kwani mwanafunzi si mwajiriwa wa serikali .

Akielezea hotuba ya Rais Kikwete juu ya walimu alisema kuwa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi imempotosha Rais juu ya madai yao isipo kuwa walimu wanachodai ni uwiano wa misharaha kati ya mtumishi wa idara nyingine ya umma mwenye elimu ya cheti na mwalimu kuwa wawe wanalipwa sawa tofauti na ilivyo sasa ambavyo mwalimu wa aina hiyo analipwa nusu ya mshahara wa mtumishi huyo wa idara nyingine ya umma.

Hata hivyo alisema kuwa walimu mkoani Iringa wataendelea na mgomo usio na kikomo hadi pale serikali itakaposikia kilio chao na kuwa hata suala la kiwango cha elimu nchini kushuka limechangiwa na serikali yenyewe kwa kutowajali walimu na kuwa hata sasa kama serikali itatumia nguvu wao kurudi kazini wote watarudi ila ufundishaji wao utakuwa ni siri yao na majibu yatapatikana katika mitahani.

Mbali ya katibu huyo wa CWT walimu mbali mbali mjini Iringa wamedai kuwa iwapo serikali itatumia nguvu wao kurudi kazini wasishangae kuona idadi ya wanafunzi wanaofeli kuongezeka zaidi.

HOTUBA YA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 JULAI, 2012


Ndugu Wananchi;

Naomba nianze kwa kuomba radhi kwa kutoa hotuba ya mwisho wa mwezi wa saba, leo tarehe 01 Agosti, 2012 badala ya jana tarehe 31 Julai, 2012. Hii ni kwa sababu ya msiba uliotukuta katika familia na mimi kwenda Lindi kushiriki maziko ya marehemu wetu. Tofauti na miezi iliyopita leo, pamoja na hotuba ya kawaida ya mwisho wa mwezi nimetoa fursa kwa Wahariri wa vyombo vya habari nchini kuniuliza maswali nami kujibu. Kwa upande wangu nina mambo matatu ambayo nitayazungumzia leo.

Ajali ya Kuzama kwa Meli ya MV SKAGIT

Ndugu Wananchi;

Jambo la kwanza ni ajali ya Meli ya MV SKAGIT iliyotokea tarehe 18 Julai, 2012. Meli hiyo ilikuwa na watu 290, wakiwemo mabaharia 9, abiria watu wazima 250 na watoto 31. Juhudi za uokoaji zilianza mara baada ya taarifa ya kuzama kwa meli hiyo kupatikana. Maofisa na askari wa JWTZ, Polisi na KMKM walishiriki pamoja na meli na watu binafsi katika uokoaji. Waokoaji walifanikiwa kuwapata ndugu zetu 146 wakiwa hai na maiti 126 hadi tarehe 27 Julai, 2012. Kwa maana hiyo basi, watu 18 hawajulikani walipo na inahofiwa kuwa nao pia hawako hai. Huenda wamezama pamoja na meli au walizama baharini lakini miili yao haikuweza kupatikana.

Ndugu Wananchi;

Napenda kutumia nafasi hii kurudia kutoa mkono wa rambirambi na pole nyingi kwa wale wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika ajali ile. Nampongeza sana Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wenzake wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa kazi kubwa na nzuri waliofanya kuongoza juhudi za uokoaji pamoja na huduma walizotoa kwa waliokolewa, waliojeruhiwa na waliofariki. Kwa wale ambao walikuwa wenyeji wa Unguja na Pemba, SMZ ilitoa sanda na usafirishaji wa maiti mpaka makwao kwa mazishi. Kwa wale wasiokuwa na ndugu Serikali ilibeba jukumu la kuwazika kule Kama, Kusini Unguja.

Natoa pongezi za pekee kwa wale wote walioshiriki katika uokoaji kwani juhudi zao ziliwezesha ndugu zetu wengi kusalimika na maiti nyingi kupatikana.

Ndugu Wananchi;

Kutokea kwa ajali ile kumetonesha jeraha la huzuni, majonzi na mashaka makubwa yaliyolipata taifa letu miezi 11 iliyopita kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spice Islander. Katika mkutano maalum wa Baraza la Usalama wa Taifa niliouitisha tarehe 20 Julai, 2012 kuzungumzia ajali ya MV SKAGIT tulifanya mapitio ya utekelezaji wa maagizo yetu ya mkutano wa tarehe 11 Septemba, 2011 kufuatia ajali ya MV Spice Islander. Kwa ujumla tumeridhika kuwa utekelezaji umekuwa mzuri kwa upande wa mamlaka zinazohusika na usafirishaji majini yaani SUMATRA, Zanzibar Maritime Authority na mamlaka za Bandari za nchi zetu mbili. Ushirikiano baina ya mamlaka hizo sasa ni mzuri kwa mambo yote muhimu ambayo Baraza liliagiza wafanye hivyo. Pamoja na hayo Baraza limetaka ushirikiano huo uzidishwe na kuimarishwa.

Kwa mfano, Baraza limefurahishwa na kupongeza kitendo cha mamlaka hizo kutumia Dar es Salaam Maritime Institute kwa ushauri kuhusu ubora wa meli na huduma za usafirishaji majini. Baraza limeagiza vyombo hivyo viwe na hadidu za rejea zinazofanana kwa vigezo vya ubora ili nchi yetu iwe na viwango vinavyofanana vya ubora wa meli na huduma za usafirishaji baharini kwa pande zetu mbili za Muungano. Bahari ni moja na vyombo vinahudumia watu wale wale, kuwa na vigezo tofauti vya ubora wa meli na viwango vya huduma ni jambo lisilostahili kuwepo tena, ni la hatari. Baraza pia limeagiza pawepo na ukomo wa umri wa meli zilizokwishatumika zinazoruhusiwa kutumika hapa nchini.

Aidha, Baraza limerudia kuagiza pawepo na usimamizi makini zaidi kuhusu upakiaji wa mizigo na abiria. Mamlaka husika, yaani SUMATRA, ZMA na maofisa wa bandari wahakikishe kuwa uwezo wa meli uliohakikiwa na kutambuliwa unaheshimiwa ipasavyo. Pia, meli zikaguliwe mara kwa mara na vigezo vifanane.


Ndugu Wananchi;

Pamoja na hayo, Baraza la Usalama wa Taifa limeona kuwa wakati umefika kwa Serikali yetu kuwa na Coast Guards, yaani kikosi maalum cha uokoaji na usalama majini. Aidha, Baraza limetaka hatua za makusudi zichukuliwe kuimarisha KMKM na Police Marines. Mwisho, Baraza lilipongeza uamuzi wa SMZ wa kuunda Tume ya kuchunguza ajali ile kama ilivyofanya wakati wa ajali ya MV Spice Islander.

Utafutaji na Uchimbaji Gesi Nchini

Ndugu Wananchi,

Jambo la pili ninalopenda kulizungumzia leo ni kuhusu maendeleo ya sekta ya gesi asili nchini. Juhudi za kutafuta mafuta nchini zilianza mwaka 1952 na mwaka 1954 wakati kampuni ya BP ilichimba kisima cha kwanza kule Mafia. Bahati mbaya kisima hicho hakikuzaa matunda yaliyotarajiwa na juhudi za utafutaji mafuta zikafifia kabisa mwanzoni mwa miaka ya 1960. Miaka kumi baadae, juhudi hizo zilianza upya na kuendelea kwa kiwango na kasi za namna mbalimbali hadi sasa. Katika miaka ya hivi karibuni juhudi zimekuwa kubwa na kuhusisha makampuni kadhaa ya kimataifa yakiwemo makubwa na madogo.

Ndugu Wananchi;

Tangu mwaka 1954, mpaka sasa visima 61 vimechimbwa, kati ya hivyo, gesi asili imegunduliwa katika visima 22, visima 14 vya nchi kavu na maeneo ya maji mafupi na visima 8 vya bahari ya kina kirefu. Hatujabahatika kupata mafuta lakini tumefanikiwa kupata gesi asili katika maeneo kadhaa baharini na nchi kavu katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo kutokana na visima vilivyochimbwa mpaka sasa, akiba ya gesi asili iliyopo nchini inakadiriwa kuwa kati ya futi za ujazo trilioni 25.4 – 28.9. Yapo matumaini makubwa ya gesi nyingi zaidi kugundulika katika miaka michache ijayo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba shughuli za utafutaji mafuta na hasa gesi baharini zilizoanza mwaka 2004 kukiwa na kampuni moja sasa zipo 18. Baada ya ugunduzi wa kwanza wa gesi mwaka 2010, shughuli za utafutaji sasa zimepamba moto na zimekuwa na mafanikio. Naamini gesi nyingi zaidi itaendelea kupatikana.

Fursa za Maendeleo

Ndugu Wananchi;

Kwa kiasi cha gesi asili kilichokwishagunduliwa na kwa matumaini yaliyopo ya gesi zaidi kupatikana kunaifanya Tanzania kuwa moja ya nchi za kutumainiwa duniani kwa upatikanaji wa gesi asili miaka michache ijayo. Hali hiyo inaipa nchi yetu fursa kubwa ya kuweza kujiletea maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii muda si mrefu kutoka sasa.

Gesi asili ni rasilimali inayoweza kutumika kuzalisha mbolea na hivyo kusaidia katika kuendeleza kilimo nchini kwa kurahisisha upatikanaji wake na kuwa ya bei nafuu. Gesi asili inaweza kutumika kuzalisha umeme na hivyo kuiwezesha nchi kupata umeme wa kutosha na kuwepo ziada ya kuuza nje. Hivi sasa, katika gridi ya taifa megawati 350 za umeme zinatokana na gesi asili na hata lengo letu la kuzalisha megawati 3,500 ifikapo maka 2015 tunategemea zaidi gesi asili kuwezesha hilo kutimia. Ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam una shabaha hiyo.


Ndugu Wananchi;

Vile vile, gesi asili inaweza kutumika kutoa nishati viwandani badala ya kutumia mafuta na hivyo kupunguza gharama za uzalishaji. Watu majumbani wanaweza kutumia gesi asili kupikia hivyo kupunguza matumizi ya umeme, mafuta, mkaa na kuni. Inapunguza gharama za maisha na kusaidia kuhifadhi mazingira kwa kupunguza ukataji wa miti. Ni kutokana na kutambua ukweli huo ndiyo maana TPDC inatekeleza mradi wa kutengeneza gridi ya mabomba ya kusambaza gesi majumbani katika jiji la Dar es Salaam.

Jambo lingine muhimu kuhusu rasilimali hii ni kwamba tukiuza nje gesi nchi yetu itapata mapato mengi tena ya fedha za kigeni. Kwa vile gesi ni nyingi mapato ya Serikali yataongezeka sana, hivyo kuijengea uwezo wa kutimiza majukumu yake vizuri zaidi. Kama matumizi yatakuwa mazuri, gesi asili itakuwa kichocheo kikubwa cha kukuza uchumi wa nchi. Maendeleo ya haraka yatapatikana na hivyo kusaidia kuwaondoa wananchi wengi kutoka katika lindi la umaskini tulionao sasa.


Changamoto Muhimu

Ndugu Wananchi;

Pamoja na ukweli kwamba kuwa na gesi asili nyingi kunaipa nchi yetu fursa kubwa ya kujiletea maendeleo, zipo pia changamoto zake. Hatuna budi kuzitambua na kuzitafutia ufumbuzi ili gesi iweze kunufaisha ipasavyo nchi yetu na watu wake. Changamoto zipo nyingi lakini kubwa zipo za namna tatu.

Changamoto ya kwanza ni ile ya kujenga uwezo wetu wenyewe wa kudhibiti shughuli zinazofanywa na makampuni ya mafuta ili tuhakikishe kuwa tunapata malipo yanayostahili. Inatulazimu tuwe na wataalamu wetu wazalendo wa fani za taaluma zihusuzo gesi kama vile uhandisi, kemia, jiofizikia, uhasibu, ukaguzi na sheria. Tusipojenga uwezo wetu wenyewe kwenye maeneo hayo kuna hatari ya kudhulumiwa na kupata hasara. Pengine ipo haja ya kuwa na chombo maalum kwa ajili hiyo kama tulivyofanya kwa mafanikio kwa upande wa dhahabu.

Changamoto ya pili ni ile ya kupata Watanzania wengi wenye ujuzi na taaluma zinazohitajika na soko la ajira la sekta ya gesi. Tusipofanya hivyo makampuni yataajiri watu hao kutoka nje na hivyo kufanya Watanzania kutokunufaika na fursa za ajira zilizopo.

Ndugu Wananchi,

Kwa changamoto hizi mbili, jawabu lipo kwenye elimu na mafunzo tunayotoa kwa vijana wetu katika shule, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya juu. Kwanza kabisa lazima tuboreshe elimu ya sayansi na hisabati katika shule zetu za msingi na sekondari. Katika vyuo vya ufundi tutoe mafundi mchundo wa taaluma zinazohitajika na tasnia ya gesi na mafuta. Hivyo hivyo kwa upande wa vyuo vikuu nako wafundishe wataalamu wa fani zinazohitajika kama vile utafutaji wa gesi na mafuta, uendelezaji wa mafuta na gesi, uchumi na biashara ya mafuta na gesi, uhasibu na ukaguzi wa mafuta na gesi pamoja na sheria za mafuta na gesi na mikataba ya utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi.

Ndugu Wananchi;

Napenda kuwahakikishia kuwa tayari tumejipanga kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinajiandaa kuanza kutoa mafunzo ya Chemical and Environmental Lab for Oil and Gas na fani ya Exploration and Production Software Technology katika mwaka huu wa masomo. Chuo cha Madini Dodoma kitaanza kutoa mafunzo ya diploma ya Petroleum Geoscience kuanzia Septemba mwaka huu. Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha, na Chuo cha Teknolojia cha Mbeya na kile cha Dar es Salaam pia wameanza kufundisha mitaala hiyo. Aidha, VETA Makao Makuu na VETA Mtwara nao wanafundisha masomo yahusuyo gesi. Wizara ya Nishati na Madini itawadhamini wanafunzi 50 kutoka Mkoa wa Mtwara kwenda kupata mafunzo hayo ya gesi asili katika chuo cha VETA Mtwara.

Ndugu Wananchi;

Wizara ya Nishati na Madini pia inatekeleza mpango mkakati wa kuwapata wataalamu wa sekta hiyo kati ya 40-50 kati ya sasa na mwaka 2016. Taaluma zinazotiliwa mkazo ni Petroleum Geoscience, Petroleum Geophysics, Petroleum Geochemistry, Petroleum Engineering, Petroleum Modeling, Oil and Gas economics, Oil and Gas Accounting and Auditing na Oil and gas Legal Regimes and Contract Negotiations. Kwa upande wake, Serikali itatoa upendeleo maalum kwa kulipia gharama zote za mafunzo ili tuweze kuwapata wataalamu hawa mapema iwezekanavyo. Nawaomba vijana wetu wachangamkie fursa hizi za masomo na watakapohitimu mafunzo wawe tayari kuitumikia nchi yetu kwa bidii.

Kujenga Uwezo Wetu wa Kutumia Mapato ya Gesi

Ndugu Wananchi,

Changamoto nyingine kubwa sana ni ile ya kuhakikisha kuwa mapato yatokanayo na gesi yanatumika vizuri na kwa manufaa ya taifa na watu wake. Lazima tuanze sasa kufikiria na kujipanga kwa ajili hiyo. Si vyema tukangojea mpaka hapo mapato yatakapoanza kupatikana ndiyo tufikirie na kutengeneza mfumo mzuri wa kusimamia na kutumia mapato yatokanayo na gesi. Tutakuwa tumechelewa, watu laghai na waovu watakuwa wameanza kunufaika hivyo watakuwa wagumu kutengeneza mfumo utakaowanyima fursa ya kuliibia taifa.

Jambo hili ni muhimu sana kufanya kwani ipo mifano hai ya nchi zenye rasilimali nyingi za mafuta na gesi lakini nchi na wananchi wake hawanufaiki sawia. Mauzo yanafanyika na fedha nyingi kupatikana lakini manufaa kwa nchi na watu wake ni madogo au hayapo kabisa. Wanaonufaika ni viongozi na baadhi ya maofisa wa umma wanaohusika na usimamizi wa shughuli zihusuzo rasilimali hizo. Na, hata sisi tunaweza kujikuta katika hali hiyo kama tusipojipanga vizuri sasa ambayo badala ya rasilimali kuwa baraka zinageuka kuwa balaa au hata laana.

Ndugu Wananchi;

Zipo nchi duniani ambazo zina usimamizi mzuri wa mapato ya rasilimali za mafuta na gesi na kuleta baraka na neema kwa taifa na watu wake. Nchi hizo zimeweza kuhifadhi na kutumia vizuri mapato yake kukuza uchumi wa nchi kwa jumla na kuboresha upatikanaji wa huduma za kiuchumi na kijamii kwa watu. Matokeo yake ni watu wa nchi hizo kuishi maisha yaliyo bora kuliko walivyokuwa kabla ya kupatikana kwa rasilimali hizo. Lakini, hii imewezekana kutokana na usimamizi mzuri na matumizi mazuri ya mapato yatokanayo na mafuta na gesi.

Tumeamua kujifunza kutoka nchi za wenzetu waliofanikiwa ili na sisi tunufaike. Na sisi tunajiandaa kutengemeza Sera ya Gesi Asili na kurekebisha Sheria ya Utafutaji na Uzalishaji wa Mafuta na Sheria ya Menejimenti ya Mapato ya Serikali yatokanayo na gesi zitakazotoa majibu hayo na kuliwezesha taifa kuwa na mfumo mzuri wa usimamizi wa utafutaji na uchimbaji wa gesi asili pamoja na usimamizi na matumizi mazuri ya mapato yatokanayo na gesi hiyo. Wapo wenzetu kwa mfano, wanacho kitu kinachoitwa Sovereign Funds ambapo mapato yote huhifadhiwa na baadae hutolewa kwa utaratibu maalum. Tunataka tujifunze kutoka kwao ili na sisi tutengeneze chombo chetu cha namna hiyo ili tunufaike.

Ndugu Wananchi;

Mambo hayo tumeshaanza kuyafanyia kazi. Katika mazungumzo yangu na baadhi ya wakuu wa nchi rafiki na mashirika ya maendeleo ya kimataifa, nimewasilisha maombi ya kusaidiwa na kushirikiana kwa mambo mawili. Kwanza kwa kuwawezesha Watanzania kupata mafunzo ya haraka kwa wataalamu watakaosaidia kusimamia shughuli za utafutaji, uendelezaji na biashara ya gesi asili nchini. Pili, watusaidie kupata watu wenye ujuzi na uzoefu ili watushauri kuhusu namna ya kutengeneza mifumo bora ya kusimamia na kutumia mapato ya gesi kwa mujibu wa mifano ya wenzetu waliofanikiwa. Nafurahi kwamba maombi yetu yamepokelewa vizuri na nchi zote na mashirika yote ya kimataifa tuliozungumza nao. Baada ya muda si mrefu kazi itaanza.

Mgomo wa Walimu

Ndugu Wananchi;

Jambo la tatu na la mwisho ni mgomo wa walimu. Pengine ni mapema kusema kwa vile kesho Mahakama itaamua kuhusu shauri hilo. Lakini napenda kuwahakikishia walimu kuwa tunawajali, tunawathamini na kutambua mchango wao muhimu kwa taifa letu. Wakati wote tumekuwa tunashughulikia madai ya haki zao na malimbikizo mbalimbali. Madai ya safari hii ni makubwa mno, yametuzidi kimo. Athari za kuyatimiza yalivyo yataifanya bajeti ya Serikali kutumia asilimia 75 kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Serikali na kubakiza asilimia 25 kwa kuendeshea Serikali na kutimiza majukumu ya maendeleo kwa wananchi. Haitakuwa sawa. Ndiyo maana tumeshindwa kuelewana walipokataa rai hiyo na wao kusisitiza kugoma.

Wakati tunaendelea kusubiri uamuzi wa Mahakama, nina maombi mawili kwa walimu: Moja, wasiwalazimishe walimu wasiotaka kugoma wafanye hivyo, wawaache waendelee na kazi. Pili, wasitumie watoto isivyostahili kujenga hoja zao. Nawasihi warudi kwenye meza ya mazungumzo.

Ndugu Wananchi;

Kabla ya kumaliza hotuba yangu naomba nitumie fursa hii kuwatakia Waislamu wote nchini kheri na baraka tele kwa swaumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhan. Wakati wote, mjiombee wenyewe kwa Mwenyezi Mungu awajaalie toba na malipo mema katika mfungo huu. Mkumbuke pia kuiombea nchi yetu amani, upendo na mafanikio mema.
Baada ya maneno hayo, naomba sasa niishie hapo. Nawashukuru sana kwa kunisikiliza. Sasa nipo tayari kujibu maswali ya Wahariri kama yapo. Ndugu Wahariri mliopo hapa, karibuni.

Viwanjani Leo Ijumaa

Naomba Kutoa Hoja ,Kuna umuhimu gani kushiriki mashindano ya kimataifa ikiwa tuna maandalizi duni?. tubadilike tujipe muda wa maandalizi tuanzishe shule za michezo za kutosha tuandae wachezaji si washiriki wa michezo(Watalii) ,Serikari sasa ni wakati wa kuwekeza kwa nguvu katika sekta ya michezo na si maandalizi ya zima moto, Wanamichezo tunasema tumechoshwa na visingizio visivyokuwa na Mashiko "Pamoja tuboreshe michezo yetu" Capt Mkami Jr

Thursday, August 2, 2012

ZAWADI YANGU YA LEO KWENU


SNOOP DOGG SASA AJIITA SNOOP-LION,AIMBA REGGAE

Inawezekana ni njia mpya ya kutaka kuteka watu na kutengeneza hela kwa aina mpya ya biashara baada ya kukaa kwenye muziki kwa miaka ishirini, huu ni uamuzi wa rapper Snoop Dogg ambae sasa amebadilisha jina na kujiita Snoop Lion ameutangaza.






Ametangaza kuanza kuimba muziki wa Reggae anaouita muziki wa upendo, muziki atakao kuwa huru kuuperform hata kwa bibi, babu na watoto kwa sababu una mapokezi kwa marika yote tofauti na muziki wake wa kigumu alioufanya kabla.






Snoop Lion amesema alichofahamu kutoka kwa Marasta ni kwamba sio dini kama watu wanavyofikiria pia kuhusu jinsi wanavyoishi, amegundua kitu kingine tofauti pamoja na kusisitiza kwamba amekua rasta kwa kipindi kirefu lakini alikua hajafungua jicho la tatu ili kuligundua hilo, ila baada ya kufungua ndio amefahamu.






Kubadili jina na kuanza kufanya muziki wa Reggae hakua amekupanga, anasema ni hisia zilikuja tu na akaamua kuzifata, baada ya hapo ndio akasafiri mkapa Jamaica na kuingia kwenye studio ambayo aliiagiza imtengenezee kazi za ukweli za Reggae ambazo alizifurahia na kuzifanyia kazi.






Snoop mwenye umri wa miaka 40 ambae kipimo cha DNA kilionyesha kwamba asili yake sio Asia bali ni Africa 75%, 23% Native American na 6% European amesema haimaanishi kwamba muziki wa rap aliokua akiufanya mwanzo ni mbaya na kwamba anauacha bali anafanya muziki ulio kwenye hisia zake kwa sasa ambao ni reggae.