Wanajeshi wa serikali ya Syria wameendelea na mashambulio yao dhidi ya maeneo
yanayodhibitiwa na wapiganaji katika mji wa Aleppo.
Inaarifiwa kuwa watu zaidi ya 30 wameuwawa.
Lakini inaonesha jeshi la ardhini la Syria halijaweza kusonga mbele katika
baadhi ya mitaa, na mwandishi wa BBC anasema, inaonesha vita vya Aleppo kwa
sasa ni vya mashambulio ya mizinga na mabomu kila baada ya muda.
Katika eneo la Deir ez-Zor, wanaharakati walisema watu 17 waliuwawa wakati
vifaru vilivopiga basi ambalo lilikuwa na watu waliokuwa wakikimbia
mapigano.
|
No comments:
Post a Comment