Tuesday, September 25, 2012

Msako dhidi ya Boko haram, 35 wauawa

Takriban wapiganaji 35 wa kundi la kiisilamu la Boko Haram, wameuawa katika msako mkali dhidi ya kundi hilo Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Kwa mujibu wa jeshi la Nigeria, wapiganaji wengine sitini walikamatwa wakati wa msako huo kwenye majimbo ya Adamawa na Yobe.
Kundi hilo la kiisilamu, linapinga mifumo ya kimagharibi na athari zake nchini Nigeria na wamekuwa wakifanya mashambulizi yanayolenga maslahi ya nchi za Magharibi pamoja na makanisa.
Mnamo siku ya Jumapili, kulitokea shambulizi dhidi ya kanisa moja katoliki na ambalo lilisababisha mauaji ya watu wawili. Boko Haram ndilo limelaumiwa kwa kufanya shambulizi hilo.
Msemaji wa jeshi nchini humo, alifahamisha shirika la habari la AFP kuwa msako huo ulifanyika usiku kucha kati ya siku ya Jumapili na Jumatatu.
Wanajeshi walifanya msako wa nyumba hadi nyumba, katika mitaa mitatu na wakati mwingine kufyatuliana risasi na wapiganaji hao, usiku kucha.
Wanajeshi wawili walijeruhiwa katika makabiliano hayo.
Bunduki na mabomu vilipatikana katika maficho ya wanamgambo hao pamoja na silaha zengine ikiwemo mishale 32 na panga.
Mji huo umekuwa mojawapo ya miji iliyoathirika sana kutokana na harakati za Boko Harama ambalo linataka kutumika kwa sheria za kiisilamu kote nchini humo.

Mapishi kando ya barabara


KIEPE NDIYO HIKI SASA


Masaibu ya watoto wa Syria

Shirika la kutetea haki za watoto Save the Children, limekusanya maelezo ya kutisha na kuogofya kuhusu visa vinavyowakumba watoto katika vita vinavyoendelea nchini Syria.
Shirika hilo limekusanya ushahidi kutoka kwa watoto waliotoroka vita na ambao wameelezea dhulma na mateso waliyokumbana nayo.
Kwa mujibu wa shirika hilo, kila mtoto aliyehojiwa na ambaye ameweza kutoroka Syria, ameelezea kuona jamaa wake angalau mmoja akiuawa.
Shirika hilo linasema kuwa limehoji mtoto mwenye umri wa miaka 15, aliyechomwa kwa sigara,wakati alipokuwa amefungwa katika iliyokuwa shule yake.
Mtoto mwingine alizungumzia kupigwa na umeme huku akiishi katika chumba kimoja na maiti.
Ingawa shirika hilo halikutoa taarifa rasmi kuhusu nani aliyetenda mateso hayo, limeisisitizia Umoja wa Mataifa kuchukua hatua dhidi ya wanaotenda dhulma hizo.

Friday, September 21, 2012

Julius Malema matatani kwa utata wake

Polisi wa Afrika Kusini wametoa waranti ya kukamatwa mwanasiasa wa Afrika kusini anayeleta utatanishi, Julius Malema, ambaye alifukuzwa kutoka chama tawala cha ANC.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani juma lijalo kuhusu mashtaka ya ku-ghu-shi fedha, rushwa, na wizi kwa njia za udanganyifu.
Kamati maalumu ya uchunguzi, iitwayo "the Hawks", imekuwa ikichunguza shughuli za kibiashara za Bwana Malema.
Bwana Malema, ambaye aliwahi kuwa mfuasi mkubwa wa Rais Jacob Zuma, amegombana na washirika wake wa zamani, na akafukuzwa chamani, kwa kutoa wito kuwa serikali ya Botswana inafaa kupinduliwa.

Arusha Wakati Wa Rufaa Ya Lema Jana











Gari ya polisi ikiwa inapisha maandamano yapite
RUFAA ya kupinga kuvuliwa ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), ambao ulikua inatarajiwa kusikilizwa leo na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa chini ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande na wenzake, Natalia Kimaro na Salum Massati umesikilizwa ila kesi imeahirishwa.

Kesi hiyo ambayo ilikuwa inatolewa maamuzi jana imeairishwa na jaji mkuu wa Tanzania kwa kile kilichodaiwa kuwa wakili wa upande wa mkata rufaa na wakili wa serekali kupata matatizo ya kufiwa na baba yao mzazi


Jaji mkuu alifikia hatua ya kuamua kesi hiyo ihairishwe hadi pale ifikapo October 2 mwaka huu ambapo ndipo imesemekana huku ya kesi hiyo ndio itakapo tolewa.
Mara baada ya kesi hiyo kuhairishwa umati mkubwa uliokuwepo mahakamani hapo uliondoka hadi katika ofisi za chama cha demokrasia na maendeleo Chadema ambapo aliyekuwa mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema aliongea na wananchi walikuwa wakimsindikiza nae aliwasihi wananchi hao kuwaombea majaji wa kesi hiyo ili waweze kutoa hukumu ya haki.

“mimi sio kwamba nataka nishinde na wala siogopi kushidwa ila naomba tuwaombe hawa majaji wa kesi hii ili waweze kutoa maamuzi ya haki yasiyomgandamiza mtu yeyote,na napenda pia kuchukuwa nafasi hi kuwaeleza kuwa jumanne tunatarajia kufanya mkutano katika kiwanja cha ngarenaro ambapo hapo ndipo tutakapo fungua kampeni zetu za udiwani rasmi”alisema lema

Alibainisha kuwa mbali na kuzindua kampeni pia wanampango wa kuzindua mikutano ambayo itajulikana kufa au kupona ,mkutano ambao utafanywa nyumba kwa nyumba pamoja na kitongoji kwa kitongoji

Kutoka JamiiForums

Mbunge Msigwa akiwa tayari kuandamana huku akitumia kiti cha wagonjwa ili kushinikiza kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa kungo'ka.


Friday, September 7, 2012

HUYU NDIO MWANAJESHI MMAREKANI ALIEANDIKA KITABU KUHUSU MAUAJI YA OSAMA.

.
Wizara ya usalama ya Marekani (Pentagon) imetishia kumpeleka mahakamani mwanajeshi alieandika kitabu kuhusu jinsi yeye na wenzake walivyomuua gaidi Osama Bin Laden aliekua kiongozi wa Al Qaeda.
Mwanajeshi huyo aliekua kwenye kundi la wanajeshi wenye ujuzi wa hali ya juu alikua mtu wa pili kuingia chumbani alipokuepo Osama ambapo kwenye kitabu alichoandika anaeleza kwamba Osama hakua na silaha yoyote walivoingia chumbani kwake, taarifa ambayo inatofautiana na iliyotolewa na Pentagon.
Kanuni zinazoongoza oparesheni kama iliyomuua Osama zinawanyima wanajeshi waliohusika kutoa siri au kutangaza chochote ndio maana anaonekana kavunja makubaliano.
Sasa hivi vyombo vya habari vimeanza kuhusisha hicho kitabu na kampeni za urais jambo ambalo mwanajeshi huyo amelikataa na kusisitiza kwamba amekiandika hicho kitabu ili kuweka hadharani ukweli bila kulenga chama chochote cha siasa wala mgombea.
Matt Bissonnette(36) ambae hafurahii uongozi wa rais Obama, alikua hataki kutambuliwa kwenye vyombo vya habari lakini tayari jina lake limeshajulikana na limesambaa hivyo ilimlazimu kujificha.

MWENYEKITI WA MBEYA PRESS KLABU CHRISTOPHER NYANYEMBE AUA UJUMBE WA BODI UTPC

mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Christopher Nyanyembe akiomba kura katika nafasi ya ujumbe wa bodi ambayo amepita kwa kura 33 kati ya 64 zilizopigwa
Bw.Deus Buganywa akiomba kura kuwa mjumbe wa bodi leo na kushinda kwa kura 26 kati ya 64 zilizopigwa hivyo kuwa mjumbe katika nafasi hiyo iliyoombwa na wajumbe 7 akiwemo Masau Bwile aliyepata kura (13),Emanuel Bwibo (15),Beny Mwaipaja (15) Andrew Kuchochoma (11)na Hashim Hasan (15)

KENETH SIMBAYA AULA TENA UTPC JANE MIHANJI AWA MAKAMU WAKE

Rais mstaafu wa Kwanza UTPC Ulimboka Mwakariri akifuatilia uchaguzi wa kidemokrasia wa UTPC
Mweka hazina wa IPC Vicky Macha (kulia) akipokea salamu za rambi rambi ndani ya ukumbi wa mkutano juu ya kifo cha mwenyekiti wake Daudi Mwangosi
Mpembea pekee wa Ally Haji Hamad ambaye ni katibu mtendaji wa Pembea Press Klabu ambaye amepita bila kupingwa leo kuwa mjumbe wa bodi mwakilishi wa Zanzibar
katibu wa IPC Frank Leonard kushoto akishuhudia Rais wa UTPC Keneth Simbaya akipongezwa



mwandishi wa mtandao huu ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Lindi Abdulaziz Video akifuatilia uchaguzi huo leo
Rais wa UTPC Keneth Simbaya (kushoto) akipongezwa na mkurugenzi wa UTPC Bw Abbakari Kasiani
Makamu wa Rais Jane Mihanji akijieleza kabla ya kuchaguliwa kwa kura za kishindo
Rais wa UTPC Keneth Simbaya akitoa neno la shukrani kabla ya kuchaguliwa tena

Rais wa UTPC Bw Simbaya akipongezwa na mjumbe wa bodi iliyopita Juma Nyumayo(kulia)
Rais wa UTPC Bw Simbaya akivunja bodi leo



Mwenyekiti mstaafu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) ambaye alimwachia kiti marehemu Daudi Mwangosi amepitishwa tena kwa kishindo katika nafasi hiyo baada ya kupata kura 60 kati ya Jane Mihanji amepata kura za hapana 2 na kura za ndio 60 kati ya kura 62 zilizopig wa katika uchaguzi huo.

Waandishi wa mtandao huu kutoka Dar es Salaam Esther Macha na Abdulaziz Video wanaripoti kuwaKatika uchaguzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Simbaya amepata kuwashukuru wajumbe kwa ushirikiano mkubwa ambao amepata kuuonyesha katika kipindi kilichopita na hivyo kuwaomba ushirikiano huo uzidi katika kipindi kichacho.

Simbaya amewataka wajumbe hao mkutano huo kuendelea kushikamana zaidi na kuwa katika uongozi wake uliopita amepata kuwa kiunganishi kizuri kati ya UTPC na wahisani kwa asilimia 150 na kuahidi kuendelea kufanya hivyo katika kipindi kijacho.

Alisema kuwa ili kuweza kusonga mbele zaidi bado UTPC inahitaji viongozi wenye mahusiano mema na wahisani ili kuiwezesha UTPC kufanya vema zaidi.

Miili Ya Askari Wa JWTZ Waliokufa Nchini Sudani Yaagwa Leo

Askari wa Jwtz wakiwa wamebeba moja ya jeneza la mwili waaskari wa 3 wa jeshi hilo waliofariki kwa ajali ya maji wakivuka mto Lamada, Sudani walikokwenda kulinda amani chini ya jeshi la umoja wa Mataifa muda mfupi kabla ya kuiaga mili hiyo Lugalo jijini Dar es Salaam
Askari wa JWT wakingiza miili ya marehemu katika Gari tayari kwa safari ya kuelekea mikoani kwa ajili ya Mazish
Mkuuwa Majeshi nchini Devis Mwamunyange akifariji mke wa moja wa askari walifariki Bi, Fatuma Chunguile


Mkuuwa Majeshi nchini Devis Mwamunyange akitoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu

Ombi la Rais Obama kwa wamarekani

Rais wa Marekani Barack Obama, amewaomba wamarekani kumpa fursa nyingine kuiongoza nchi hiyo.
Ombi lake amelitoa katika kilele cha kongamano la chama cha Democratic mjini North Carolina.
Akijiwasilisha kama mgombea wa urais mwenye kuleta matumaini kwa wamarekani, Rais Obama alisema kuwa uchaguzi utakaofanyika mwezi Novemba, utatoa fursa kwa wapiga kura kuchagua kati ya maono mawili tofauti kuhusu hatma ya Marekani.
Aliwataka Wamarekani kuwa wavumilivu akisema kuwa matatizo yanayokabili Marekani yamekuwa yakiongezeka kwa miaka mingi na kuwa itachukua muda kuweza kuyatatua.
Lakini aliongeza kuwa ikiwa watamchagua tena, ataweza kubuni nafasi mpya za kazi, kupunguza madeni na kuimarisha uchumi wa Marekani.
Rais Obama alisema anajiona kama kiongozi aliyekuwa amewekwa kwa mizani kujaribiwa uongozi wake na kuwa amefaulu. Alisema mpinzani wake wa Republican, Mitt Romney, hayuko tayari kwa mashauriano ya kidiplomasia.
Alitofautisha malengo yake na yale ya chama pinzani na kurejelea kauli mbiu yake ya mwaka 2008 , kuwataka watu kuwa na matumaini.
"sikuwahi kusema kuwa safari hii itakuwa rahisi na sitatoa ahadi hiyo hii leo'' Obama aliambia kongamano la wajumbe wa Democrat.
Mitt Romney wa chama cha Republican atapambana na Rais Obama kuwania urais huku kura za maoni zikionyesha wawili hao wakikaribiana.

Mashambulizi ya kulipiza kisasi Kenya


 
Takriban watu kumi na moja wa kabila la Pokomo wameuawa katika mashambulizi mapya ya kulipiza kisasi katika eneo la Tana River,Kusini Mashariki mwa Kenya.
Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo alisema alisikia watu wakipiga mayowe wakati kijiji kimoja kilipokuwa kinashambuliwa na kisha wenyeji kuteketezwa.
 
Eneo hilo ambako zinaishi jamii za kuhamahama ni kitovu cha mizozo ya ardhi na maji kati ya jamii za Orma na Pokomo.
Watu wengine kumi walijeruhiwa kwenye uvamizi huo uliotokea usiku wa kuamkia leo.
Uvamizi huu umetokea baada ya mashambulizi mengine kutokea mwezi jana ambapo watu 52 kutoka jamii ya Orma wengi wakiwa watoto na wanawake kuuawa kwa kunyongwa na kuteketezwa kiasi cha kutotambulika.
Ni katika tukio ambalo lilitajwa kuwa ghasia mbaya za kikabila kutokea katika miaka ya hivi karibuni nchini Kenya. Polisi na viongozi wa kijamii walisaidia kutuliza hali na kurejesha usalama kati ya jamii hizo mbili lakini hali ya wasiwasi iimeendelea kutanda.
Licha ya kwamba polisi waliahidi kuimarisha hali ya usalama katika eneo hilo, viongozi wa eneo hilo wanasema vikosi vya usalama vimeshindwa kuzuia ghasia.
Mbunge wa eneo hilo, Danson Mungatana amewashtumu maafisa wa usalama kwa kushindwa kuchukua hatua za kuwalinda wananchi licha ya kufahamu mapema kwamba mashambulio yatatokea.
Jamii hizo mbili za Pokomo na Orma, zimekuwa zikizozana kuhusu matumizi ya ardhi na maji ambazo ni rasilimali adimu.
Wapokomo ni wakulima ambao hukuza chakula kando ya mto Tana wakati jamii ya Orma wakiwa wafugaji wa kuhamahama.

Wednesday, September 5, 2012

WAANDISHI WA HABARI WAMLIA NGUMU MANUMBA


Wanahabari Iringa wakiwa katika ukumbi wa ofisi ya RPC leo

Katibu wa Iringa Press Club Frank Leonard akiwasilisha msimamo wa wanahabari kwa DCI Manumba.
Mmiliki wa mtandao huu Francis Godwin akiwa na mkewe wakitoka katika ofisi ya RPC baada ya Manumba kushindwa kufuata msimamo uliotolewa na wanahabari wa Iringa.
DCI Robert Manumba akiongea na waandishi Iringa leo
Waandishi wa habari wa Iringa wakiwa katika ofisi ya RPC leo
WAANDISHI wa Habari wa mkoani Iringa wamekataa kupokea kupokea taarifa ya awali ya uchunguzi ya mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi iliyofanywa na jeshi hilo iliyokuwa itolewe jana na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba.
Hatua hiyo imekuja baada ya Manumba kukataa kuwaondoa katika mkutano wake na waandishi wa habari maafisa wa jeshi la Polisi wanaofanya kazi mkoani hapa huku kukiwepo na tamko la waandishi hao kusitisha kufanya nao kazi ya kihabari mpaka tume huru zilizoundwa zitakapotangaza matokeo ya uchunguzi wao.
Pamoja na wanahabari kukataa kupokea taarifa hiyo, Manumba alikanusha taarifa zingine zinazodai kuwepo kwa waandishi wa habari wawili wanaodaiwa kuwepo katika mpango wa kuuawa na baada ya mmoja wa wanahabari hao Francis Godwin kujisalimisha na kumuhoji sababu za kutakiwa ajisalimishe polisi.
Katika kikao hicho kilichoitishwa majira ya saa sita mchana katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, wanahabari walionesha msimamo wao kwa kumtaka Manumba awatoe maafisa wa jeshi hilo wa mkoani hapa.
“Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Iringa walikwishatangaza katika tamko lao kwamba wamesitisha ushirikiano wa kihabari na jeshi hilo la Polisi mkoani hapa mpaka pale tume huru zilizoundwa kuchunguza kifo cha mwanahabari huyo zitakapotoa majibu yao,” alisema Frank Leonard ambaye ni Katibu Mtendaji wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa.
Leonard alimwambia Manumba kwamba waandishi wa habari hawana tatizo lolote na yeye na kwamba wapo tayari kupokea taarifa yake hiyo ya uchunguzi ila kwa sharti kwamba ni lazima maafisa polisi wote wanaofanya kazi mkoani hapa na ambao walikuwepo katika chumba hicho cha mikutano watoke.
“Huu ni msimamo wetu, hatupo tayari kufanya kazi na maafisa wa jeshi lako na tunamuomba IGP Said Mwema ampumzishe kazi kwa muda Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa bwana Michael Kamuhnada mpaka pale tume huru zilizoundwa zitakapotoa taarifa za matokeo ya uchunguzi wao,” Leonard alisema alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya tamko la wanahabari hao.
Akiwasihi wanahabari kushirikiana na jeshi la Polisi, Manumba alisema mara baada ya mauaji hayo kutokea jeshi la Polisi makao makuu liliunda tume ya uchunguzi akiwemo yeye mwenyewe ambayo kwa kiasi kikubwa imeifanya kazi hiyo.
“Leo nilikuwa nataka niwape taarifa ya uchunguzi ya mauaji hayo, lakini kwa sharti mnalonipa sidhani kama hilo litawezekana,” alisema.
Alisema kila mtu ameguswa na mauji ya Mwandishi huyo na kwamba kosa lililofanywa na wahusika haliwezi kuwa kosa la kila mtu.
Bila kufafanua Manumba alisema matukio ya aina hiyo yapo katika jamii yetu, na yanaweza kuendelea kutokea ikiwa ni pamoja na kwake au maafisa wa jeshi hilo.
“Jambo hili baya limetokea na sisi Polisi tuna regret na hata serikali ina regret, ndio maana tume iliundwa na mara moja tukakimbia kuja hapa ili kupata ukweli baada ya kupeleleza na tukaona ni vizuri uchunguzi tuliofanya tuutoe kwenu” alisema.
“Hata hivyo kwa kuwa huu ni msimamo wa waandishi na wote mmeuunga mkono mbele yangu, nadhani uchunguzi uliofanywa na jeshi letu itabidi upitiwe na tume nyingine badala ya kuutoa kwenu,” alisema.
Hata alipoombwa akatoe taarifa ya uchunguzi huo ambayo hata hivyo baadhi ya wanahabari walisema inaweza kuwa na lengo la kuvuruga ushahidi unaokusudiwa kukusanywa na tume zingine ikiwemo ile iliyoundwa juzi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Emanuel Nchimbi, DCI alisema tume iliyoundwa na waziri inatakiwa iachwe ifanye kazi yake kwahiyo itapata fursa pia ya kupitia uchunguzi wao huo.
Katika kipindi hiki kigumu kwa wanahabari na wadau mbalimbali wa tasnia hiyo, Manumba alisema yapo mengi yatakayozungumzwa kuhusu kifo cha Mwangosi zikiwemo taarifa za uzushi, za kupikwa na za ukweli.
Kuhusu kuwepo kwa taarifa ya orodha ya waandishi wahabari wengine wawili wanaotakiwa kushughulikiwa na jeshi hilo, Manumba alisema hazina ukweli kwani mbali na kufanya kazi na wadau wengine, jeshi hilo linawategemea sana wanahabari katika kazi zake.
“Kwahiyo ndugu zanguni mkutano umefungwa na sasa tuiache tume ifanye kazi yake,” alisema.

Michelle Obama amuombea mumewe kura


 
Mkewe Rais wa Marekani, Barack Obama, Michelle, amehutubia kongamano la chama tawala cha Democratic ambapo alitetea haki ya mumewe kupewa nafasi kutawala taifa hilo kwa muhula wa pili.
Akiongea Kaskazini mwa Jimbo la Carolina, alimtaja mumewe kama mtu anayeelewa matatizo yanayowakumba wamarekani.
Alitetea hatua ya mumewe ya kuanzisha mpango maalumu wa bima ya afya ulioleta utata mwingi sana hasa miongoni mwa wanachama wa chama cha upinzani cha Republican walioupinga.
Alisema kuwa mumewe alinuia kutoa nafasi sawa ya matibabu kwa wote. Hata hivyo alikiri kuwa mageuzi aliyoahidi mumewe miaka minne iliyopita yalikuwa magumu kuyatekeleza lakini akasisitiza kuwa yatafaulu baadaye.
Rais Obama atahutubia kongamano hilo baadaye juma hili, ambapo atakubali rasmi kuwa mgombea wa Urais wa chama cha Democratic.

PICHA ZA MAZISHI YA DAUDI MWANGOSI

.
.
.
.
.
.
Mke wa Marehemu.
.
Watoto wa marehemu.
.
Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa.
.
.
Picha zote zimepigwa na mbeyayetu.blogspot.com
Marehemu Daudi Mwangosi.