Monday, November 12, 2012

.Polisi 40 wauawa na wezi wa mifugo Kenya

 
Takriban polisi 40 wamethibitishwa kuuawa nchini Kenya katika shambulizi lililofanywa dhidi yao siku ya Jumamosi walipokuwa wanajaribu kuokoa mifugo waliokuwa wameibwa.
Maafisa hao walivamiwa katika eneo la Baragoi, kaunti ya Samburu, Kaskazini mwa nchi.

Msemaji wa polisi aliambia BBC kuwa polisi 29 waliuawa pamoja na washambuliji watatu , lakini viongozi wa kijiji wanahofia kuwa huenda maiti zaidi wakapatikana. Hii leo miili zaidi ilipatikana na kufikisha idadi ya polisi waliouawa kuwa 40.

Wenyeji wa eneo hilo wana historia ya kupigana kwa sababu ya uhaba wa malisho ya mifugo wao

Wiki mbili zilizopita, watu 12 waliuawa katika shambulizi kama hilo kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya.

Haya yanasemekana kuwa mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kutokea dhidi ya polisi tangu Kenya kujipatia uhuru wake.

Maiti 11 walipatikana siku ya Jumamosi na wengine 19 kupatikana Jumapili.

Ramani ya Kenya

Inspekta wawili wakuu wa polisi wangali hawajulikani waliko.

Uvamizi huu ni pigo kubwa kwa idara ya ulinzi nchini. Baadhi ya polisi waliviziwa na kuuawa na wezi wa mifugo, katika eneo la Lomerok. Manusura tisa wangali wanapokea matibabu hospitalini.

Mauaji haya yanafikisha idadi ya watu waliouawa katika eneo hilo katika wiki mbili zilizopita hadi 43.

Aidha mashambulizi haya yanatokea huku shughuli ya kuajiri inspekta mkuu wa polisi ikiendelea sambamba na polisi kususia kazi kwa sababu ya mzozo wa mishahara.

HII NDIO GENERATOR INAYOTUMIA HAJA NDOGO (MKOJO)


moja kati ya product ambayo haikutegemewa kabisa ni hii ya Genereta inayotumia haja ndogo (Mkojo) katika Maker Faire Africa mwaka huu huko Lagos Nigeria iliyotengenezwa na watoto wakike wanne ambao ni Duro-Aina Adebola (14), Akindele Abiola (14), Faleke Oluwatoyin (14) na Bello Eniola (15).



Lita moja ya mkojo inakupa masaa 6 ya umeme



Mfumo mzima unafanya kazi hivi:


  • mkojo unawekwa kwenye electrolytic cell ambayo inatenganisha Hydrogen
  • Hydrogen inakwenda kwenye filter ya maji kwa ajili ya kusafishwa ambapo baada ya hapo inasukumwa kwenda kwenye gas cylinder.
  • Gas cylinder inaisukuma Hydrogen kwenye cylinder ya liquid borax ambayo inatumika kuondoa moisture kwenye gas ya hydrogen
  • hii gas ya Hydrogen iliyosafishika inasukumwa na kuelekea kwenye generetor

MTOTO WA MIAKA MITATU ACHOMWA MOTO KISHA KULAZIMISHWA KULA KINYESI CHAKE MAJENGO JIJINI MBEYA


 
MTOTO ANETH AKIWA AMEOKOLEWA NA WASAMARIA WEMA HUKO MAJENGO

HIVI NDIVYO ALIVYOUNGUZWA MTOTO ANETH NA MAMA YAKE MDOGO

HUYU NDIYO MAMA MDOGO WA ANETH AMEJULIKANA KWA JINA LA BAHATI LUKANGARA NDIYO ALIYEMUUNGUZA MTOTO ANETH


HAPA MAJIRANI WAKIJARIBU KUMUULIZA SABABU ZA KUMUUNGUZA HUYO MALAIKA WA MUNGU NINI SABABU YAKE MPAKA AKACHUKUA HATUA YA KUMUUNGUZA LAKINI KWA KIBURI CHA HUYO MAMA ALIKAA KIMYA KABISA BILA YA KUJIBU CHOCHOTE

MWENYEKITI WA MTAA HUO HABIBA MWAKITALU AMEMBEBA MTOTO ANETH TAYARI KWA KUMPELEKA HOSPITALI HUKU NYUMA AKIFUATIWA NA MWESHIMIWA DIWANI KATA YA MAJENGO SAMWELI

WANANCHI WENYE HASIRA KALI WALIMCHUKUA MAMA HUYO NA KUMPELEKA KITUO CHA POLISI


MTUHUMIWA NA MGONJWA WANAINGIZWA KATIKA GARI LA MWESHIMIWA DIWANI TAYARI KWA KUPELEKWA POLISI

Katika hali isiyo ya Kawaida Mkazi wa majengo jijini Mbeya Ndugu Bahati Rukangara amemchoma moto mtoto mdogo wa mika 3 aliyefahamika kwa jina la Aneth kisha kumfungia Ndani na kumlazimisha ale kinyessi chake.

Akizungumza Mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu Habiba Mwakitabu amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 10 :30 asabuhi ambapo majirani na mwanamke huyo waligundua mara baada ya kusikia sauti ya mtoto huyo akilia kutokana na maumivu.

Amesema mara baada ya kusikia sauti hiyo walifika eno hilo na kunza kumhoji ili kufahamu kiini cha tatizo hilo ambapo alishindwa kutoa ushirikiano ndipo walipo anza kumpiga .
Amesema kutokana na hali hiyo majirani walilazimika kubomoa mlango ndipo walipo mkuta mtoto huyo akiwa uchi huku ameungua vibaya mwilini hasa katika upande mmoja eneo la mkono wa kushoto .

Amesema mara baada ya kumhoji mtoto huyo aliwaeleza kuwa mama yake mdogo alichukua nguo na mkumfunga mkononi kisha kumwagia maji ya moto pamoja na kumlazimisha ale kinyesi chake hali ambayo iliwafanya washindwe kuvumilia na kuanza kupiga kelele kwa lengo la kuomba msaada kwa watu wengine.

Kwa mujibu maelezo ya mwenyekiti huyo amesema kuwa Mtuhumiwa huyo amekuwa akifanya vitendo vya manyanyaso kwa mtoto huyo marakwamara ambapo wamekuwa wakimuonya lakini amekuwa si mtu wa kusikia.
Ameesema mtoto huyo si wa kwa kwakwe kwani amekuwa akiishi naye kwa muda mrefu sasa ambapo aliachiwa na dada yake ambaye hakufahamika kuwa nayishi wapi kwa sasa.

Hata Diwani wa kata hiyo Ndugu Samuel Mamboma alifika eneo hilo tukio na kutoa msaada wa usafiri kwa lengo la kumfikisha mama huyo polisi pamoja na mtoto huyo ambaye naye alikimbizwa Hospitali.
Hata hivyo amesema tukio hilo si la kwanza kutokea katika meaeno hayo kwani kumekuwepo na matukio mengi hasa ya utoaji mimba na kutupwa watoto.

PICHA KWA HISANI YA KALULUNGA
HABARI KWA HISANI YA EMANUEL MADAFA

Tuesday, November 6, 2012

WAAFRIKA SEHEMU MBALI MBALI WASHEREHEKEA OBAMA KUSHINDA TENA URAIS


Barack Obama aibuka mshindi

 
Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Marekani yameanza kutolewa kutoka maeneo mbali mbali ya nchi.
Rais Barack Obama ameshinda katika majimbo ambayo yalikuwa muhimu sana kubaini mshindi wa uchaguzi huu ambayo ni Michigan na Pennsylvania, pamoja na mengine ambayo alishinda katika uchaguzi wa mwaka 2008.
Mwenzake wa Republican Mitt Romney ameshinda katika majimbo mengine muhimu pia ya Republican pamoja na kushinda Indiana ambalo lilimuunga mkono Obama mwaka 2008.
Mamilioni ya watu walijitokeza kupiga kura siku ya Jumanne. Mshindi huenda akajulikana baada ya masaa kadhaa kuanzia sasa hususan huku matokeo katika majimbo mengine muhimu yakitolewa.
Kura za maoni kabla ya kufanyika uchaguzi huu zilionyesha kinyang'anyiro kitakuwa kikali ingawa zilimpa ushindi wa kura chache tu Rais Obama katika majimbo kadhaa muhimu.
Vituo vya kupigia kura vilianza kufungwa mapema katika maeneo ya Mashariki mwa nchi , huku majimbo ya Virginia na Ohio nayo yakifunga mapema.
Kwa sasa kura za Electoral College zinaonyesha Obama yuko nyuma ya Romney kwa kura sita

AKINA MAMA,WATOTO KWA RAHA ZAO

Akina mama ambao majina yao hayakufahamika mara moja walikutwa na mmiliki wa Blog hii jana jioni maeneo ya Mshindo Manispaa ya Iringa wakiendelea na mazungumzo yao kwa mbwembwe bila huku wakiwa wamekalia moja ya kaburi kati ya makaburi mengi yaliyopo maeneo hayo.

Matokeo yaanza kutolewa Marekani


Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Marekani yameanza kutolewa kutoka maeneo mbali mbali ya nchi.
Rais Barack Obama ameshinda katika majimbo ambayo yalikuwa muhimu sana kubaini mshindi wa uchaguzi huu ambayo ni Michigan na Pennsylvania, pamoja na mengine ambayo alishinda katika uchaguzi wa mwaka 2008.
Mwenzake wa Republican Mitt Romney ameshinda katika majimbo mengine muhimu pia ya Republican pamoja na kushinda Indiana ambalo lilimuunga mkono Obama mwaka 2008.
Mamilioni ya watu walijitokeza kupiga kura siku ya Jumanne. Mshindi huenda akajulikana baada ya masaa kadhaa kuanzia sasa hususan huku matokeo katika majimbo mengine muhimu yakitolewa.
Kura za maoni kabla ya kufanyika uchaguzi huu zilionyesha kinyang'anyiro kitakuwa kikali ingawa zilimpa ushindi wa kura chache tu Rais Obama katika majimbo kadhaa muhimu.
Vituo vya kupigia kura vilianza kufungwa mapema katika maeneo ya Mashariki mwa nchi , huku majimbo ya Virginia na Ohio nayo yakifunga mapema.
Kwa sasa kura za Electoral College zinaonyesha Obama yuko nyuma ya Romney kwa kura sita
 
Kwa hisani ya BBCswahili

Noti mpya zenye sura ya Mandela A Kusini

Noti mpya zenye sura ya Mandela
 
 
Noti za kwanza zilizo na uso wa rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, zimeanza kutumika nchini humo.
Ni noti za kwanza za Afrika Kusini kuwa na uso wa kiongozi mweusi na zinachukua mahala pa noti zilizokuwa na nyuso za wanyama na picha za viwanda.
 
Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma anasema kuwa noti hizo zilikuwa kama ishara ya shukrani kwa Mandela.
Bwana Mandela, mweye umri wa miaka 94, ni mmoja wa watu wanaoenziwa sana duniani baada ya kufungwa jela miaka 27 alipokuwa anapigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Gavana wa benki kuu Gill Marcus alikuwa wa kwanza kutumia noti hiyo kwa kununua bidhaa katika duka moja mjini Pretoria.
Alisema kuwa bwana Mandela ana furaha kuona noti hiyo.
Pia alielezea kuwa Afrika Kusini hujaribu kila baada ya miaka saba kubadili sarafu yake ya noti kwa sababu za kiusalama.
Sura ya Mandela iko upande mmoja wa noti hizo mpya wakati wanyama wakubwa watano Simba, Kifaru, Chui , Ndovu na Nyati, wakiwa upande wa pili.
Alishinda tuzo la amani la Nobel mwaka 1993 kwa sababu ya harakati zake dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi na kuchaguliwa rais mwaka uliofuata kabla ya kujiondoa mwenyewe mamlakani baada ya kipindi kimoja tu cha utawala wake.
Akisifika sana kwa jina lake "Madiba", amestaafu kutoka kwenye ulingo wa siasa
 
Kwa hisani ya BBCSWAHILI.COM.

Polisi walifanya udanganyifu A. Kusini

Watu wanaounga mkono polisi kuwajibishwa juu ya mauaji ya wachimba migodi
 
 
Maafisa wa polisi nchini Afrika kusini wameshutumiwa kuweka silaha karibu na miili ya wachimba migodi waliouawa karibu na mgodi wa palatinum wa Marikana.
Picha zilizowasilishwa mbele ya tume inayochunguza mauaji hayo zinaonekana kudhibitisha tuhuma hizi.
Picha moja inaonyesha mwili wa mwanamume aliyefariki katika sehemu iliyo karibu na mgodi wa Marikana.
Picha ya pili iliyopigwa baadaye lakini siku hiyo hiyo, ni sawa na picha ya kwanza lakini hii inaonyesha mwanamume yuyo huyo akiwa na panga lenye mkono wa rangi ya manjano lililo chini ya mkono wake wa kulia.
Picha zote zilipigwa na maafisa wa polisi wa Afrika kusini muda mfupi tu baada ya kuuawa kwa wachimba mgodi thelathini na wanne na polisi mnamo mwezi Agosti.
Kuna mifano zaidi.Hili lina maana kuwa eneo la tukio la uhalifu huenda lilibadilishwa na maafisa hao wa polisi ili kushinikiza kujitetea kwao kuwa waliwashambulia wachimba mgodi hao ili kujikinga.
Ushahidi unazuka katika tume inayochunguza mauaji hayo ya Marikana. Wakili George Bizos ambaye kwa wakati mmoja alimtetea Nelson Mandela, anasema kuna ushahidi mzito wa kujaribu kuzuia haki kutendeka.
Alitoa wito kwa maafisa wakuu wa polisi kueleza ni nini kilichofanyika.
 
Kwa hisani ya BBCSWAHILI.COM

Monday, November 5, 2012

Uchaguzi waanza nchini Marekani

Rais Barack Obama ametoa wito wake wa mwisho kwa wapiga kura katika mkutano wa hadhara mjini Iowa huku wamarekani wakijitokeza kupiga kura kuamua ikiwa atapata muhula wa pili au mpinzani wake Mitt Romney ndiye atachukua usukani katika ikulu ya White House.

Mwandishi wa BBC ambaye yuko kwenye kampeini ya Romney, anasema kuwa hizi dakika za mwisho ni kuhusu kuwashawishi wapiga kura katika uchaguzi huu wenye ushindani mkali

Kura za kwanza zimepigwa katika jimbo la New Hampshire, ambako inaarifiwa Obama na Romney wamepata kura tano kila mmoja kati ya kura kumi. Kura hizi hazitokani na wapiga kura kwa ujumla bali watu maalumu ambao huteuliwa kupiga kura katika kile kinachojulikana kama Electoral village.

 

Kwa hisani ya BBCSWAHILI.COM


Askari wa Rwanda wamuua mwanajeshi wa DRC

Rwanda imetuhumu wanajeshi kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kufanya uchokozi baada ya kundi moja kuvuka mpaka.
Hali iliyosababisha makabiliano katika eneo tete la mpakani kati ya nchi hizo mbili. .
Mmoja wa wanajeshi wa Congo alipigwa risasi wakati mmoja wa Rwanda alijeruhiwa katika ufyatulianaji wa risasi. Tarrifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa jeshi.
Msemaji wa jeshi la DRC alidokeza kuwa makabiliano yalikuja baada ya wanajeshi wa DRC kuvuka mpaka kununua vileo.
Rwanda imekuwa ikikana kuhusika na vita vinavyoendelea Mashariki mwa DRC lakini wafadhili kadhaa wamesitisha msaada kwa Rwanda baada ya Umoja wa Mataifa kutoa madai kuwa wanawapa silaha waasi na kufadhili kundi la M23.
Takriban watu 500,000, wametoroka makwao Mashariki mwa DRC tangu mwezi Aprili,wakati kundi la M23 lilipoanza mapigano.
Mwandishi wa BBC Jean-Claude Mwambutsa nchini Rwanda anasema kuwa hii ndio mara ya kwanza kutokea makabiliano kati ya wanajeshi wa Rwanda na DRC tangu mwaka 2001.
Anasema kuwa huku jamii ya kimataifa ikiwa imezipiga darubini nchi hizi mbili, sio rahisi hatua kama hii kusababisha vita.
Msemaji wa jeshi la Rwanda, Brigedia Generali Joseph Nzabamwita, alisema wanajeshi kutoka DRC walikuwa wanaingia DRC kufanya uchunguzi.
"Hiki ni kitendo cha uchokozi. Wanataka kingiza Rwanda katika shida zao za ndani lakini Rwanda imekuwa ikisema haiko tayari kuchochea hali hiyo," alisema Brigedia Nzabamwita.
Makabiliano hayo yaliripotiwa kutokea karibu na eneo la Kibumba, kilomita kumi na tatu Kaskazini mwa mji wa Goma.

KHADIJA KOPA ALIVYOFUNIKA MITIKISIKO YA PWANI DAR LIVE



Malkia wa mipasho nchini, Khadija Kopa, kutoka T.O.T akiwapagawisha mashabiki waliohudhuria Mitikisiko ya Pwani Dar Live Jumamosi.
MALKIA wa mipasho nchini, Khadija Kopa, juzi (Jumamosi) alifunika vilivyo katika Tamasha la Mitikisiko ya Pwani lililofanyika ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.



Khadija Kopa na vijana wake wakiwa wameiteka Dar Live kwa burudani.
Tamasha hilo lilipambwa na makundi mbalimbali ya taarab yakiwemo Jahazi, Coastal, TOT na mengineyo. Watangazaji mahiri kutoka Times Radio wakiongozwa na Gardner G Habash na Khadija Shaibu 'Dida' walinogesha tamasha hilo na kulifanya liwe la kipekee.



Kiongozi wa Kundi la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf 'Mfalme', akiimba na mashabiki wake.


Mke wa Mfalme, Leila Rashid, akilipamba Tamasha la Mitikisiko ya Pwani ndani ya Dar Live.


Mwanahawa Ally wa East African Melody akiwarusha mashabiki wa Mitikisiko ya Pwani.


Kiongozi wa kundi la Mashauzi Classic, Isha Ramadhan 'Isha Mashauzi', akiwapa raha mashabiki.



Maua Tego wa Coastal Modern Taarab akiwa stejini.


Sehemu ya mashabiki waliofurika Dar Live kushuhudia tamasha hilo.


Khadija Kopa na wasanii wenzake wa TOT wakilitawala jukwaa.


Wasanii wa TOT wakizidi kunogesha tamasha hilo.


Mzee Yusuf akimchombeza mkewe, Leila Rashid.


Mashabiki wa Arsenal nao walikuwepo.


Wapenzi wa taarab waliokuwa VIP wakifuatilia tamasha hilo.


Isha Mashauzi akionyesha mbwembwe zake stejini.


Mashabiki waliopanda stejini kumtunza Mzee Yusuf wakijiachia kwa raha zao.


Nyomi iliyohudhuria Tamasha la Mitikisiko ya Pwani.

(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL)

MABINGWA WA BALIMI BOAT RACE MWANZA WAPATIKANA

Wapiga makasia 15 wakinyosha makasia yao juu kabla ya kuanza kwa fainali za mashindano ya mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) yaliyofanyika jijini Mwanza jana.



Mabingwa wa ngoma za asili wa mashindano ya ngoma ya kanda ya ziwa kikundi cha Bujora wakitumbuiza mashabiki wa mashindano ya mitumbwi yaliyofanyika jana kwenye fukwe za Mwaloni Mkoani Mwanza jana ambapo washindi watakao wakilisha mkoa huo kwenye fainali wamepatikana.



Msanii wa kikundi cha ngoma cha Bujora akichezea nyoka kwa kuingiza kichwa mdomoni wakati wakitumbuiza watu waliofika kushuhudia mashindano ya mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) yaliyofanyika Mwaloni Mkoani Mwanza jana

Mashindano Ya Kusaka Vipaji Ya Kabati Katiba Star Search Iringa Yafikia Patamu


 Majaji  wa  shindano  ya Kabati katiba star search wakiwa katika  picha ya pamoja na mdhamini mkuu  wa mashindano hayo mbunge wa  viti maalum mkoa  wa Iringa Ritta Kabati (CCM) wa  pili  kushoto ,wengine ni Agnes Muba Temy Mahondo na jaji mkuu Edo Bashir ( wa  pili kulia) na jaji mwingine  ni Dj Yeyo hayupo  pichani 
 Mmoja kati ya  washiriki  akionyesha  uwezo  wake katika  shindano hilo la kabati katiba Search  ambalo lipo kwa ajili ya  kuibua vipaji vya  wasanii mkoani Iringa
Hawa  ndio  walioingia katika  kinyang'anyiro cha kuwasaka  wasanii wasanii 10 kati ya 25 waliopita awamu ya kwanza

Shindano la  kuwasaka  wasanii  wasanii  bora 10 kati ya 25  walioingia katika mchuano wa  kusaka tuzo maalum ya mbunge wa viti maalum mkoa  wa Iringa Ritta Kabati (CCM) kupitia  shindano lake alililibuni na kulipa  jina la kabati katiba  Star Serach limefanyika leo katika ukumbi  wa Twistars mjini Iringa. 

Akizungumza na mtandao       wa  www.francisgodwin.blogspot.com ,mratibu  mkuu  wa shindano  hilo Rashid Msigwa amesema kuwa  tayari  wasanii 10  wamepatikana kwa ajili ya  kuingia hatua ya fainali katika  shindano hilo ambalo amedai kuwa  limekuwa na mvuto  zaidi .

Msigwa amesema  kuwa  awali  wasanii  walikuwa  wakionyesha uoga katika jukwaa ila kwa sasa  wameonyesha  kujiamini  zaidi.

Aliwataja  wasanii  walioingia hatua ya  fainali  leo kuwa ni  Alfred Madembwe,Adimaya Mlawa,Humphrey Sambala,Mohamed  Mpangala, Jackson Mam,Henry Said, Edga Bosco , Emmanuel Mgata , Julius Kimata na Adam Kayombo.

Huku Jaji mkuu  wa shindano hilo Edo Bashir akieleza  kufuruhishwa kwake na jinsi ambavyo  wasanii  hao  wanavyojituma katika  jukwaa na kuwa  upo uwezekano  wa mkoa wa Iringa  kupitia shindano hilo  kutoa  wasanii bora  zaidi ambao  wanaimba vizuri kuliko hata  wasanii  wakubwa hapa nchini.

Sudan Kusini yamfurusha afisaa wa UN

Sudan Kusini imemfukuza afisaa mmoja wa Umoja wa Mataifa aliyekuwa anachunguza hali ya haki za binadamu.
Msemaji wa serikali anasema kuwa afisaa huyo alichapisha ripoti ya uchunguzi wake ambayo haikuwa na ukweli
Maafisa wa umoja wa mataifa wamekosoa hatua hiyo wakisema kuwa ilikiuka majukumu ya nchi hiyo ya kisheria.
Kufukuzwa kwa afisaa huyo, walisema kunaweza kuhusishwa na ripoti iliyochapishwa mwezi Agosti na ambayo ilishutumu jeshi kwa kutesa, kufanya ubakaji , mauaji na utekaji nyara.
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wametoa madai sawa na hayo dhidi ya nchi hiyo ambayo ilijipatia uhuru wake kutoka kwa Sudan mwezi Julai mwaka jana.
Mchunguzi huyo wa umoja wa mataifa, alitajwa na maafisa wa umoja wa mataifa kama Sandra Beidas.
Msemaji wa serikali Barnaba Marial Benjamin alisema kuwa afisaa huyo aliripoti madai ambayo hangeweza hata kuthibitisha na amekuwa akizichapisha ripoti zake bila sababu.
"Hili ni jambo linalokiuka maadili’’ alisema bwana Marial bila kufafanua zaidi.
Hilde Johnson, mkuu wa ujumbe wa vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Sudan, aliitaja hatua hiyo ya kufurushwa kwa mjumbe huyo kama kuhujumu sheria ya serikali chini ya makubaliano ya umoja wa mataifa.
Alisema kuwa alitaka serikali kutoa maelezo kuhusu hatua hiyo.
"Kuchunguza hali ya haki za binadamu na kuripoti na vile vile kuwezesha mashirika ni mojawapo ya majukumu ya jeshi la UNMISS ambalo linapaswa kulindwa ," alisema afisaa huyo.
Mwezi jana shirika la, Amnesty International lilichapisha ripoti iliyotuhumu wanajeshi wa serikali kwa kufanya vitendo vya kushangaza vya ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo mauaji na ubakaji.
Serikali ilijibu kwa kupuuza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu akisema vilikuwa visa ambavyo havikutarajiwa.

Sunday, November 4, 2012

HUYU NDIO MISS TANZANIA 2012.

Brigitte Alfred ndie mshindi kati ya washiriki wenzake 29.
.
.
.
Mshindi wa Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred (katikati)katika picha ya pamoja na mshindi wa Pili Eugene Fabian (kushoto) na Mshindi wa Tatu, Edda Sylvester, Brigitte anatokea Kitongoji cha Sinza na Kanda ya Kinondoni wakati, Eugene Mkoa wa Mara na Kanda ya Ziwa, Edda ni Miss Kigamboni na Kanda ya Temeke.
.
.
.
.
.
.
.
Picha zote zimepigwa na Mrokim wa http://mrokim.blogspot.com
Waendesha shughuli Jokate pamoja na Taji Liundi.