Monday, July 9, 2012

Wazazi/Walezi: Kisa hiki kinawahusu

Mkasa huu umesimuliwa na rafiki wa karibu tarehe 7 Julai 2012, nauweka hapa kwa ajili ya Wazazi/Walezi kutilia maanani:
---
Jana nilipata kisa kilichotokea kwa rafiki yangu mmoja hivi, ni noma.

Ni nyumba ya kupanga, ina sehemu 2 ambayo familia 2 tofauti zinaweza kukaa. Familia moja (my friends') ina mtoto wa kiume wa almost miaka 2, familia ya pili ni ya mke na mume na mdogo wao mmoja mvulana ana miaka kati ya 19 - 20. Hii familia ya pili hawana house girl, ile yenye mtoto wana housegirl.

Ikatokea housegirl anahitaji kitu dukani, akaona amuache mtoto kwenye nyumba ya pili (house mates) ambako anamkuta huyo kijana wa miaka 19 na kumuomba amuache mtoto mara moja... jamaa akakubali.

Msichana wa kazi akaenda zake dukani, huku nyuma mama mwenye mtoto akarudi home na kukuta mtoto yuko kwa jirani na hapo hapo housegirl akarudi pia.

Wakamwacha tu kwa jirani, lakini baada ya muda mama mtoto akasikia mtoto analia kidogo, akamwambia housegirl amchukue. Akamchukua, then wakati jioni anaogeshwa, ndiyo wakakuta kumbe kwenye anal region kuna michubuko... wakakimbia hospitali bila kufikiria kumkamata kijana mara moja.

Somehow kijana akajua wameenda hospitali, akajua lazima itakuwa ni ishu hiyo, akasepa. Mpaka leo hajulikani alipo.

Let's be careful with our kids and those around them.

CHANZO: freebongo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment