HAPO
zamani za kale, kulikuwa na shida kubwa sana ya maji katika nchi zote. Kwa
bahati, likabakia ziwa moja tu. Wanyama wengi wa kila aina walipata maji yao
kwenye ziwa hilo. Wanyama wakubwa kama vile Tembo, Simba na Chui;
waliwanyanyasa sana wanyama wadogo waliofika kunywa maji kwenye ziwa hilo.
Wakawa hawana raha. Walipata maji kwa shida sana baada ya manyanyaso makali.
Sungura alipoona hivyo, alianza kukuna kichwa akifikiri jinsi ya kuepukana na adha hiyo. Akapata njia. Alitengeneza ngoma na kucheza kwa siri nyumbani kwake. Wanyama wengine waliposikia sauti ya ngoma ile ilivyosikika vizuri, wakavutiwa nayo. Wa kwanza kuvutiwa, walikuwa wanyama wakubwa. Wakamwendea Sungura ili wapate kuiona ile ngoma inayotoa sauti nzuri. Sungura akawaambia: “Mimi napiga ngoma hiyo na kucheza peke yangu kwa siri. Ninyi mkitaka kuiona, naomba mje mmoja mmoja, nami nitawaonyesha.” Hiyo ilikuwa mbinu yake tu kutaka kujua nani atakuwa wa kwanza na wa mwisho kuja kwake ili apate kuwatenda vibaya.
Tembo alikuwa wa kwanza kwenda kwa Sungura. Akamwambia: “Ingia nyumbani mwangu”. Tambo bila kukawia akaingia ndani. Loo, maskini Tembo! Sungura akafunga mango kwa Nguvu, mara akachoma nyumba yote. Tembo akafa.
Akaja Chui, bila kufahamu kilichotekea kwa Tembo. Yeye akapelekwa kwenye mlima wa mawe wenye mtelemko mkali. Sungura akamwambia: “Hapa wanapatikana wanyama wengi sana. Unisaidie kuwinda ili upate kula karamu kabla ya kucheza ngoma. Wanyama wanapatikana kwa urahisi sana ukifuata taratibu nitakayokuelekeza. Nayo ni hii: Ufumbe macho mpaka mnyama anapoanza kukupita. Kisha, ufumbue macho na umfuate kwa nyuma. Ndipo utakapofaulu kumkamata”.
Chui akakubali. Sungura akapanda mlimani kuporomosha jiwe kubwa. Likaja moja kwa moja kutoka juu na kumponda Chui aliyefumba macho kungoja mnyama. Sungura akamchukua Chui na kumchuna ngozi. Zamu ya Simba ilifika, akamwmbia: “Ngoma hii kila atazamaye, lazima achunwe ngozi kama walivyofanya wenzako. Tazama, ngozi hii ni ya nani? Si ya Chui?” Simba akakubali. Akachunwa kwa tamaa ya kutazama ngoma, akafa. Sungura Akava ngozi hizo kwa zamu ili kwenda ziwani kuwatishia wanyama wadogo. Sungura akatawala maji yale, wakati Wote wa shida, kutokana na werevu wake.

Hadithi
hii tamu yenye mafunzo mengi, nilipata
kuiona katika wavuti na ilielezwa kuwa imetungwa na Kat.V:A Ndunguru.
Kwa
mtazamo wangu,sungura hapa ni shujaa,alitumia akili yake kuweza kupata maji
ambayo yalikuwa bidhaa adhimu kwa wanyama wengi wadogo.
Hebu
tuangalie,maisha yetu watanzania wakawaida na ya baadhi ya viongozi wetu
tuliowachagua wenyewe kutuongoza.
Wengine
wanaishi kama miungu watu,hawaguswi,hawasogelewi,wanatunyanyasa na sisi
tunalalamika tu.Hatuchukui hatua.
Tunafahamu
fika habari za baadhi ya wabunge wetu kuwa na viburi kwa wapiga kura kiasi cha
kufikia kusema kwenye kampeni “Mnichague msinichague mimi ni mbunge wenu tu”
Haya
ni manyanyaso kama ambayo walifanyiwa sungura na wanyama wenzake wadogo.
Tofauti
yetu na sungura ni,sisi si wajanja kama yeye.Sisi ni wapole ,lakini si wakimya
kwa sababu ni mabingwa wa kulalamika.
Hakuna
lolote la maendeleo tulilofanyiwa na mbunge au diwani wetu kwa kipindi chote
cha uongozi wake,lakini akija na kipande cha sabuni tu wakati wa
uchaguzi;tunamkubali,tunamchagua tena tunaendelea kulalamika.Basi mchezo wetu
ni huo.
Ninafikiri
tujifunze kwa sungura kwani,hakuwa tayari kupewa bakuli au ndoo ya maji kwa
siku moja ili awaone akina simba,tembo na wanyama wengine wakubwa ni watu wema.
Tutumia
ngoma,tuwaalike ngomani,waje,tumalize jeuri zao wale wote wanaotufanya
tuteseke.Tuwapigie kura ya siyo,ambayo maumivu yake kwao itakuwa kama kifo.
Ngoma yetu ni uchaguzi,uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ,
tunauelekea sasa.Tufanye kweli.

No comments:
Post a Comment