MAHAKAMA
ya hakimu mkazi mkoani Singida, imeteketeza kilo 350 za bangi
aliyokamatwa nayo Pascal Bangii(31), Wilaya Nzega Mkoani Tabora, na
kukiri kosa lake kabla ya kuhukumiwa miaka kumi jela.
Uharibifu
huo umefanywa kwenye viwanja vya Mahakama chini ya hakimu Chiganga
Tengwa, Flora Ndale na ulinzi mkali wa jeshi la Polisi, Mjini Singida,
huku ukishuhudiwa na baadhi ya Wananchi.
Kijana
Bangii alikamatwa na Polisi Juni 29, 2012, baada ya kupokea taarifa
kutoka kwa raia wema, wakati akisafirisha bangi hiyo yenye thamani ya
Sh. 5,250,000, kwenda Dar es Salaam, kwa kutumia usafiri wa basi.
Aliyetoa
hukumu hiyo ya kifungo cha miaka kumi jela ni hakimu Chiganga
Tengwa, na alifanya hivyo baada ya mshitakiwa huyo kukiri mara tatu
na hivyo kupigwa faini ya Sh. Milioni 15 au kifungo cha miaka kumi
gerezani.
|
No comments:
Post a Comment