Rais wa Ghana John Atta Mills amefariki ghafla wakati akipata
matibabu.
Taarifa kutoka afisi ya rais zinasema kuwa alifariki ghafla baada ya
kupelekwa hospitali siku ya Jumatatu usiku.
Msaidizi wake pia amethibitisha kufariki kwa kiongozi huyo.
Kifo cha rais wa taifa la pili duniani kwa ukuzaji wa cocoa kimekuja wakati
alikuwa anajiandaa kupogania tena urais.
Rais Attah Mills ambaye husafiri mara kwa mara kwenda ng'ambo kwa matibabu
alifariki muda mfupi baada y kupelekwa katika hospitali moja mjini Accra ,
Ghana.
Ni hivi majuzi tu rais huyo alisafiri hadi Marekani kwa kile kilichosemekana
kwa ni uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
Kwa muujibu wa katiba ya Ghana, Makamu wa Rais John Dramani Mahama
anatarajiwa kushikilia hatamu za uongozi hadi uchaguzi wa urais
utakapofanywa.
Ghana ilikuwa inatarajiwa kwenda katika uchaguzi mkuu mwezi Disemba mwaka huu
ambapo John Attah Mills alikuwa ametangaza nia yake ya kutetea uadhifa wake.
Wakati wa uongozi wake, uchumi wa Ghana uliimarika na demokrasia kupanuka
zaidi.
" Ni kwa masikitiko makuu na kwa moyo mzito... Tunatangaza kifo cha ghafla
cha rais wa jamhuri ya Ghana " taarifa iliyotumiwa shirika la Reuters kutoka
ofisi ya rais ilisema.
Tarifa hiyo ilisema kuwa Rais Mills mwenye umri wa miaka 68 alifariki saa
chache tu baada ya kupelekwa hospitali.
Hata hivyo hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.
Lakini msaidizi wake mmoja ambaye hakutaka kutajwa, alisema kuwa Rais John
Attah Millis alisikika siku ya Jumatatu akilalamika kwa anaumwa.
Hali yake ilizorota na hatimae kufariki mapema siku ya Jumanne.
Mills , anajulikana kwa kuanzisha uchimbaji wa mafuta nchi Ghana.
|
No comments:
Post a Comment