Monday, October 14, 2013

Dk Slaa arejea Tanzania baada ya kumaliza ziara nchini Marekani

zzzw.slaaorig_eb0cb.jpg
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Dk Wilbrod Slaa leo Jumapili 13 Oktoba amesafiri kurudi Tanzania baada ya ziara yake iliyomchukua wiki tatu nchini Marekani.
Dk Slaa aliwasili nchini Marekani tarehe 21 Septemba 2013 akiambatana na mkewe mama Josephine Mushumbuzi na kupokelewa na Uongozi wa Chadema DMV.
Tarehe 22 Septemba 2013 Dr Slaa alifanya mkutano uliojumuisha wanajumuia ya Watanzania waishio katika Majimbo ya Washington, Maryland na Virginia.(P.T)
Katika ziara yake Dk Slaa alitembelea majimbo ya North Carolina na Alabama ambako alitembelea Vyuo Vikuu na Taasisi mbalimbali na kujifunza Shuguli nyingi za Maendeleo katika Sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Afya, Nishati na Uchumi.
Akizungumza akiwa uwanja wa Ndege wa Dulles mjini Washington Dk Slaa alisema alichojifunza akiwa Marekani anatarajia kupeleka maarifa hayo Tanzania ili yaweze kumkomboa Mtanzania kutoka katika Umaskini. Moja katika mambo ambayo amejifunza ni namna ya kutumia nishati ya Jua kuzalisha umeme hasa kwa wakazi wa Vijijini.
Dk Slaa amekamilisha ziara yake ya wiki tatu nchini Marekani iliyopewa jina la "Vision Tanzania" baada ya kualikwa na Umoja wa Vyuo vikuu nchini Marekani.
Taarifa hii imetolewa na waratibu wa CHADEMA Blogs

Sunday, October 13, 2013

Utalii umeingiza Trilioni ngapi kwa Tanzania? Idadi ya watalii je?


Utalii 2  Unaambiwa Utalii nchini Tanzania kwa mwaka 2012 peke yake umeingiza shilingi Trilioni 2.69 kwenye pato la taifa ikiwa ni ongezeko la asilimi 24 ikilinganishwa na mwaka 2011.
Jingine la kufahamu ni kwamba, Watalii wanaotembelea Tanzania kutoka nje ya nchi idadi yao imekua ikiongezeka kila mwaka kutoka Watalii laki nane na elfu 67,994 mwaka 2011 mpaka milioni moja na elfu sabini na saba 58 mwaka 2012.
Philiph Chitaunga ambae ni meneja wa huduma za utalii kutoka bodi ya utalii Tanzania amesema sasa hivi kuna mpango maalum kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko Tanzania.

www.millardayo.com

MBIO ZA MWENGE WA UHURU ZAMALIZIKA ,MKOA WA IRINGA WAKABIDHI TAIFANI ASUBUHI YA LEO

 Mwenge  wa uhuru  ukiwasili katika uwanja wa  kilele  cha mbio za mwenge kitaifa  uwanja wa Samora  ukitokea  viwanja  vya mkesha  Mwembetogwa ambako ulikesha kwa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa
 Viongozi  wa  serikali ya mkoa wa Iringa na  wananchi wakisubiri kupokea mwenge  kutoka Manispaa ya Iringa  leo
 Ulinzi  mkali uwanja  wa samora  leo
 Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma kulia akipokea  mwenge  kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Leticia  Warioba baada  ya Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa kumaliza mbio  hizo kwa kuzindua miradi 8  yenye thamani ya Tsh milioni 940.2
 Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dr Ishengoma  akiwa amepokea mwenge  huo tayari kluukabidhi Taifa
 Viongozi wa Kitaifa  wakiongozwa na waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Dr Fenela Mkangala wa  tatu  kulia  wakisubiri  kukabidhiwa mwenge leo  uwanja wa samora
 Mkuu  wa mkoa  wa Iringa Dr Ishengoma akisoma taarifa ya miradi iliyopitiwa na mbio za mwenge mwaka 2013
 Mkuu wa mkoa  wa Iringa Dr Ishengoma  akijiandaa kumkabidhi mwenge  waziri Dr Mkangala  leo uwanja  wa Samora
 Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma kulia akimkabidhi mwenge wa uhuru waziri Dr Mkangala  leo  uwanja  wa Samora kabla ya  waziri  huyo kuukabidhi mwenge  huo kwa vijana ili kuja kuukabidhi kwa rais Dr Kikwete kwa kuuzima mapema leo

 Waziri Dr Mkangala  akivipongeza  vyombo vya ulinzi mkoa  wa Iringa
 kamanda  wa polisi mkoa  wa Iringa  Ramadhan Mungi kulia akimpongeza mkuu wa FFU mkoa wa Iringa S.A Mnunka kwa kazi nzuri ya kukimbiza mwenge  vizuri mkoa wa Iringa



Waziri Dr Mkangala kulia akiwa na viongozi wa mkoa  wa Iringa  leo

Chanzo: www.matukiodaima.com