Baadhi ya wanaijeria waishio nje ya nchi wamejikuta wakiwa na maisha magumu
kiasi cha kuamua kuuza figo zao ili waweze kuishi. Biashara hiyo iliyoshamiri kwenye mtandao
imewafanya baadhi yao kutafuta soko la viungo hivyo muhimu kwenye mwili wa
binadamu na wengine wakisafiri hadi Malaysia na India kuuza figo zao zote mbili
kwa $30,000.
Kwa
mujibu wa mtandao wa nigeriafilms.com, watafiti wake wamebaini kuwa kuna mtandao
mkubwa sana wa wafanyabiashara, mawakala, wauzaji wa watafutaji wa bidhaa hiyo
ambao hutafuta watu watakaouza figo zao.
Wengine hufikia hatua za kuteka watu na kuwanyofoa
figo zao ili kujipatia maisha mazuri na ya haraka.
Kuna taarifa kuwa watu wengine hupoteza maisha
wakati wa oparesheni ya kunyofoa figo hizo.
Mpaka sasa karibu wanaijeria 1000 wana matumaini ya
kupata connection hizo ili nao waweze kuuza figo zao na kujipatia maisha
wanayoyataka.
Mtandao huo umemaliza
kwa kusema, “Hivi ndivyo umaskini unaosababishwa na uongozi mbovu umeifikisha
Nigeria.”
|
No comments:
Post a Comment