Kwa mara ya pili
kwenye maisha yake ya soka - kocha mkongwe Luis Van Gaal hatimaye amepata nafasi
ya kusahihisha makosa yake aliyoyafanya miaka sita iliyopita kwa kuiongoza
Uholanzi kukosa nafasi ya kucheza kwenye kombe ladunia kwa mara ya
kwanza.
Siku kadhaa baada ya
kocha Bert van Marwijk kujiuzulu kuifundisha Uholanzi baada ya kucheza kwa
kiwango kibovu kwenye Euro 2012, leo hii amepata mrithi wake - Luis van
Gaal.
Van Gaal kocha wa
zamani wa Ajax, Barcelona na Bayern Munich anamrithi Bert, huku ikiwa ni kipindi
chake cha pili kuiongoza Holland.
Baada ya
kutambulishwa kwa waandishi wa habari Van Gaal alisema: "Ni changamoto
niliyokuwa nikiisubiri sana, nashukuru nina nafasi ya kurekebisha palipoenda
vibaya mara mwisho nilivyokuwa mwalaimu wa timu ya taifa."
Kocha huyu mwenye
miaka 60 amesaini mkataba wa ambao utampeleka mpaka kwenye fainali za kombe la
dunia 2014.
|
No comments:
Post a Comment