Lawrance Mtatifiko (30)
Pichani
ni Lawarance Mtatifikolo (30) Mkazi wa Image wilayani Kilolo, mkoani
Iringa ambapo leo mtuhumiwa huyo Mtatifikolo amefikishwa katika
Mahakama ya Hakim Mkazi wa Wilaya ya Mjini Iringa akituhumiwa kufanya
fujo kinyume cha sheria ya makosa ya jinai kifungu namba 170 cha Kanuni
ya Adhabu.
Katika mahakama hiyo ilielezwa kwamba mnamo Julai 8,
mwaka huu , Mtatifiko akiwa na wenzake wanne (hawajakamatwa) walifanya
kitendo kisichoruhusishwa kisheria kwa kufunga mlango wa kanisa na
kusababisha usumbufu kwa waumini.
Walifunga lango kuu la
kuingilia Kanisa Kuu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya
Iringa wakilenga kufikisha ujumbe kwa Askofu wa Dayosisi hiyo kwamba
hawataki aendelee kuwa kiongozi wao kwasababu anatuhuma nyingi za
kimaadili na uongozi.
Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Festo
Lwila itatajwa tena mahakamani hapo Julai 24 wakati uchunguzi wake
ukiendelea.C{na Frank Leonard blog)
|
No comments:
Post a Comment