Polisi nchini Kenya wanasema watu kama 7 wamejeruhiwa kwenye shambulio la
guruneti dhidi ya kanisa katika mji wa Garissa.
Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya na televisheni ya Kenya, KTN, wanasema
idadi ya watu waliojeruhiwa inaweza kuwa kubwa zaidi na baadhi ya majeruhi ni
mahatuti.
Afisa mmoja amesema kanisa hilo lilikuwa ndani ya kambi ya polisi na guruneti
liling'oa paa wakati wa ibada.
Wengi waliojeruhiwa ni askari polisi.
Mji wa Garissa uko karibu na mpaka wa Somalia.
Mwezi wa Julai watu 15 walikufa katika mashambulio kama hayo dhidi ya
makanisa mjini Garissa.

No comments:
Post a Comment