Rais Barack Obama ametoa wito wake wa mwisho kwa wapiga kura katika mkutano wa
hadhara mjini Iowa huku wamarekani wakijitokeza kupiga kura kuamua ikiwa atapata
muhula wa pili au mpinzani wake Mitt Romney ndiye atachukua usukani katika ikulu
ya White House.
Mwandishi wa BBC ambaye yuko kwenye kampeini ya Romney, anasema kuwa hizi
dakika za mwisho ni kuhusu kuwashawishi wapiga kura katika uchaguzi huu wenye
ushindani mkali
Kura za kwanza zimepigwa katika jimbo la New Hampshire, ambako inaarifiwa
Obama na Romney wamepata kura tano kila mmoja kati ya kura kumi. Kura hizi
hazitokani na wapiga kura kwa ujumla bali watu maalumu ambao huteuliwa kupiga
kura katika kile kinachojulikana kama Electoral village.
Kwa hisani ya BBCSWAHILI.COM
|
No comments:
Post a Comment