Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Marekani yameanza kutolewa
kutoka maeneo mbali mbali ya nchi.
Rais Barack Obama ameshinda katika majimbo ambayo yalikuwa muhimu sana
kubaini mshindi wa uchaguzi huu ambayo ni Michigan na Pennsylvania, pamoja na
mengine ambayo alishinda katika uchaguzi wa mwaka 2008.
Mwenzake wa Republican Mitt Romney ameshinda katika majimbo mengine muhimu
pia ya Republican pamoja na kushinda Indiana ambalo lilimuunga mkono Obama mwaka
2008.
Mamilioni ya watu walijitokeza kupiga kura siku ya Jumanne. Mshindi huenda
akajulikana baada ya masaa kadhaa kuanzia sasa hususan huku matokeo katika
majimbo mengine muhimu yakitolewa.
Kura za maoni kabla ya kufanyika uchaguzi huu zilionyesha kinyang'anyiro
kitakuwa kikali ingawa zilimpa ushindi wa kura chache tu Rais Obama katika
majimbo kadhaa muhimu.
Vituo vya kupigia kura vilianza kufungwa mapema katika maeneo ya Mashariki
mwa nchi , huku majimbo ya Virginia na Ohio nayo yakifunga mapema.
Kwa sasa kura za Electoral College zinaonyesha Obama yuko nyuma ya Romney kwa
kura sita

No comments:
Post a Comment