Majaji wa shindano ya Kabati katiba star search wakiwa katika picha ya pamoja na mdhamini mkuu wa mashindano hayo mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) wa pili kushoto ,wengine ni Agnes Muba Temy Mahondo na jaji mkuu Edo Bashir ( wa pili kulia) na jaji mwingine ni Dj Yeyo hayupo pichani
Mmoja kati ya washiriki akionyesha uwezo wake katika shindano hilo la kabati katiba Search ambalo lipo kwa ajili ya kuibua vipaji vya wasanii mkoani Iringa
Hawa ndio walioingia katika kinyang'anyiro cha kuwasaka wasanii wasanii 10 kati ya 25 waliopita awamu ya kwanza
Shindano la kuwasaka wasanii wasanii bora 10 kati ya 25 walioingia katika mchuano wa kusaka tuzo maalum ya mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) kupitia shindano lake alililibuni na kulipa jina la kabati katiba Star Serach limefanyika leo katika ukumbi wa Twistars mjini Iringa.
Akizungumza na mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com ,mratibu mkuu wa shindano hilo Rashid Msigwa amesema kuwa tayari wasanii 10 wamepatikana kwa ajili ya kuingia hatua ya fainali katika shindano hilo ambalo amedai kuwa limekuwa na mvuto zaidi .
Msigwa amesema kuwa awali wasanii walikuwa wakionyesha uoga katika jukwaa ila kwa sasa wameonyesha kujiamini zaidi.
Aliwataja wasanii walioingia hatua ya fainali leo kuwa ni Alfred Madembwe,Adimaya Mlawa,Humphrey Sambala,Mohamed Mpangala, Jackson Mam,Henry Said, Edga Bosco , Emmanuel Mgata , Julius Kimata na Adam Kayombo.
Huku Jaji mkuu wa shindano hilo Edo Bashir akieleza kufuruhishwa kwake na jinsi ambavyo wasanii hao wanavyojituma katika jukwaa na kuwa upo uwezekano wa mkoa wa Iringa kupitia shindano hilo kutoa wasanii bora zaidi ambao wanaimba vizuri kuliko hata wasanii wakubwa hapa nchini.





No comments:
Post a Comment