Malkia wa
mipasho nchini, Khadija Kopa, kutoka T.O.T akiwapagawisha mashabiki
waliohudhuria Mitikisiko ya Pwani Dar Live Jumamosi.
MALKIA
wa mipasho nchini, Khadija Kopa, juzi (Jumamosi) alifunika vilivyo katika
Tamasha la Mitikisiko ya Pwani lililofanyika ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar
Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.
Khadija Kopa na
vijana wake wakiwa wameiteka Dar Live kwa burudani.
Tamasha
hilo lilipambwa na makundi mbalimbali ya taarab yakiwemo Jahazi, Coastal, TOT na
mengineyo. Watangazaji mahiri kutoka Times Radio wakiongozwa na Gardner G
Habash na Khadija Shaibu 'Dida' walinogesha tamasha hilo na kulifanya liwe la
kipekee.
Kiongozi wa
Kundi la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf 'Mfalme', akiimba na mashabiki
wake.
Mke wa Mfalme,
Leila Rashid, akilipamba Tamasha la Mitikisiko ya Pwani ndani ya Dar
Live.
Mwanahawa Ally
wa East African Melody akiwarusha mashabiki wa Mitikisiko ya
Pwani.
Kiongozi wa
kundi la Mashauzi Classic, Isha Ramadhan 'Isha Mashauzi', akiwapa raha
mashabiki.
Maua Tego wa Coastal Modern Taarab akiwa
stejini.
Sehemu ya
mashabiki waliofurika Dar Live kushuhudia tamasha hilo.
Khadija Kopa na
wasanii wenzake wa TOT wakilitawala jukwaa.
Wasanii wa TOT
wakizidi kunogesha tamasha hilo.
Mzee Yusuf
akimchombeza mkewe, Leila Rashid.
Mashabiki wa
Arsenal nao walikuwepo.
Wapenzi wa
taarab waliokuwa VIP wakifuatilia tamasha hilo.
Isha Mashauzi
akionyesha mbwembwe zake stejini.
Mashabiki
waliopanda stejini kumtunza Mzee Yusuf wakijiachia kwa raha
zao.
Nyomi
iliyohudhuria Tamasha la Mitikisiko ya Pwani.
(PICHA ZOTE NA
RICHARD BUKOS / GPL)
No comments:
Post a Comment