Jeshi la Uganda limesema kuwa helikopta zake nne zilizokuwa
zime ripotiwa kutoweka zikiwa njiani kuelekea nchini Somalia sasa zimepatikana
na marubani wake wote wako salama.
Akizungumza na BBC msemaji wa jeshi hilo Kanali Felix Kulaigye hakuweza
kusema ndege hizo ziko wapi kwa sasa.
Naye msemaji wa jeshi la Kenya, Bogita Ongeri ameiambia BBC kwamba operesheni
ya kutafuta ndege hizo ilikuwa imevurugwa na hali mbaya ya hewa na kuongeza kuwa
helikopta hizo nne zilikuwa kwenye safari hiyo kutoka nchini Uganda.
Moja ya helikopta hizo ilitua katika mji wa Garissa.
Rubani aliyekuwa kwenye helikopta ya pili alizungumza na mamlaka za kenya
akisema yuko katika eneo la mlima kenya lakini hakukukuwa na mawasiliano na
helikopta nyingine mbili.
Helikopta hizo za Uganda hutumiwa kusindikiza misafara kutoka angani, katika
opereresheni za utafutaji na uokoaji pamoja na kushambulia wanamgambo wa
kiislamu wa Al Shabaab nchini Somalia.
Helikpta hizo ni miongoni mwa ndege ambazo zilikuwa zikielekea Somalia kukipa
nguvu kikosi cha Umoja wa Afrika .
Awali msemaji wa jeshi la Uganda Kanali Felix Kulayigye alikuwa amesema kuwa
walikuwa wakizitafuta ndege zao mbili aina ya Mi-24 . Alisema ndege hizo ni zile
za kufanya mashambulizi.
|
No comments:
Post a Comment