Uingereza imeandika barua kwa ubalozi wa Ecuador mjini London ikitaka kurejelea
mazungumzo kuhusu hatma ya Julian Assange, mwanzilishi wa mtandao wa kufichua
siri wa Wikileaks, aliyetorokea katika majengo ya ubalozi huo kuepuka kurejeshwa
nchini Sweden kwa lazima.
Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ulivurugika baada ya uamuzi wa Ecuador
kumpa bwana Assange hifadhi ya kisiasa na Uingereza kutishia kuvamia ubalozi huo
na kumkamata.
Afisi inayoshughulika na masuala ya kigeni haijasema chochote kuhusu ujumbe
uliokop kwenye barua hiyo lakini afisa mmoja ameelezea kuwa inanuia kutuliza
hali kati ya mataifa hayo mawili.
Rais Rafael Correa ameiambia BBC kuwa Uingereza ilifanya makosa makubwa kwa kutishia kuingia kwa nguvu kwenye ubalozi
wa Equador,''Huu ni mvutano ambao ungeisha iwapo Uingereza ingetoa hakikisho ya
kupita kwa usalama kwa Bwana Assange au unaweza kuendelea kwa miezi na hata
miaka iwapo hataweza kutoka kwenye ubalozi wetu hapa London kuelekea
Equador.''
Huenda mataifa ya Amerika Kusini yakamuunga mkono rais Rafael Correa.
Huku Uingereza ikisema kuwa inataka kurejelea mashauriano kuhusu hatma ya
Julian Assange, Equador haikubaliani na msimamo huo na inataka kuhakikishiwa
kuwa Assange hatakamatwa iwapo atatolewa kwenye ubalozi wao nchini Uingereza
kuelekea Equador.
Equador inataka pia kuhakikishiwa kuwa mwanzilishi huyo wa mtandao wa Wiki
Leaks hatawahi kupelekwa Marekani anakokabiliwa na tuhuma za kutoa taarifa
muhimu na za siri kwenye mtandao wake.
Hata hivyo hakuna matumaini kwamba Marekani itakubali hilo.
Kwa hiyo ubalozi wa Equador umekiri kuwa huenda ukampa bwana Assange hifadhi
kwa miaka mingi.
|
No comments:
Post a Comment