Katibu wa CWT mkoa wa Iringa Bi.Veronica Mlungu
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kulihotubia Taifa na kuzungumzia mgomo wa walimu unaoendelea ,chama cha walimu Tanzania (CWT) mkoa wa Iringa kimeibuka na kudai kuwa Rais Kikwete amepotoshwa juu ya madai ya walimu na kuwa wanachotaka walimu kuona haki ya misharaha kwa watumishi wote inazingatiwa si vinginevyo .
Huku kikiwaonya walimu walimu ambao ni wanachama wake kuwaCWT hakitakuwa tayari kuwasaidia walimu ambao wanaendelea na kazi iwapo wataharibu mali za shule ama kuwaadhibu wanafunzi na wazazi wakachukua hatua ya kuwafungulia mashtaka katika vyombo vya sheria.
Kauli hiyo imetolewa leo na katibu wa CWT mkoa wa Iringa Veronica Malungu alipozungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuhusiana na hotuba ya Rais Kikwete kwa Taifa juu ya mgomo huo wa walimu pamoja na malalamiko ya wazazi mkoani Iringa kwa badhi ya shule ambazo zimegoma huku walimu wake wakiendelea kuwacharaza fimbo na kuwapa adhabu kali wanafunzi.
Alisema kuwa CWT kama viongozi wa walimu hao iliwataka walimu wote kugoma na baada ya kugoma asiwepo mwalimu wa kwenda shule kufundisha hadi serikali itakaposikiliza kilio chao ,ila iwapo wapo walimu wanaokwenda shule na kuwaadhibu wanafunzi kama sehemu ya kulipiza hasira zao dhidi ya serikali kuwa hilo ni kosa na wakachukulia hatua hakutakuwa na utetezi wala msaada wowote toka CWT.
Kwani alisema kuwa makubaliano ya walimu wote ni kutofika kazini wala kukanyaga maeneo ya shule kujihusisha na wanafunzi hadi serikali itakapowasikiliza hivyo ni kinyume na makubaliano kuona baadhi ya walimu wachache wakikiuka makubaliano hayo na kuhamishia hasira zao kwa wanafunzi.
Pia alisema ni kosa kwa walimu ambao hawapo katika mgomo huo kuwatumikisha wanafunzi kazi za kufundisha wenzao kwani mwanafunzi si mwajiriwa wa serikali .
Akielezea hotuba ya Rais Kikwete juu ya walimu alisema kuwa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi imempotosha Rais juu ya madai yao isipo kuwa walimu wanachodai ni uwiano wa misharaha kati ya mtumishi wa idara nyingine ya umma mwenye elimu ya cheti na mwalimu kuwa wawe wanalipwa sawa tofauti na ilivyo sasa ambavyo mwalimu wa aina hiyo analipwa nusu ya mshahara wa mtumishi huyo wa idara nyingine ya umma.
Hata hivyo alisema kuwa walimu mkoani Iringa wataendelea na mgomo usio na kikomo hadi pale serikali itakaposikia kilio chao na kuwa hata suala la kiwango cha elimu nchini kushuka limechangiwa na serikali yenyewe kwa kutowajali walimu na kuwa hata sasa kama serikali itatumia nguvu wao kurudi kazini wote watarudi ila ufundishaji wao utakuwa ni siri yao na majibu yatapatikana katika mitahani.
Mbali ya katibu huyo wa CWT walimu mbali mbali mjini Iringa wamedai kuwa iwapo serikali itatumia nguvu wao kurudi kazini wasishangae kuona idadi ya wanafunzi wanaofeli kuongezeka zaidi.
No comments:
Post a Comment