Ndege za kijeshi kutoka Marekani
zimetekeleza mashambulizi tisa ya angani dhidi ya wanamgambo wa Islamic
State kazkazini mwa Iraq ili kuvisaidia vikosi vya Iraq kuliteka bwawa
moja muhimu karibu na mji wa Mosul.
Bwawa hilo ndio kubwa nchini humo na lilitekwa na islamic state mapema mwezi huu.
Makamanda wa Marekani wamesema kuwa mashambulizi
hayo yalioanza ijumaa usiku yaliharibu zaidi ya magari 14 ya kivita
yanayomilikiwa na Islamic State.
Duru mjini Mosul zimearifu kuwa takriban wapiganaji kumi na moja wanadaiwa kuuawa katika shambulizi hilo.
Jenerali mmoja wa vikosi vya Kikurdi kazkazini
mwa Iraq amesema kuwa vikosi hivyo vimeanzisha mashambulizi ya kuliteka
bwawa hilo
CHANZO: http://www.bbc.co.uk/swahili/habari
No comments:
Post a Comment