Mkutano wa kimataifa unaoazimia
kumaliza mzozo wa Syria unafanywa mjini Geneva, huku bado kukiwa na
tofauti baina ya Urusi na mataifa ya magharibi, kuhusu jee rais wa Syria
anafaa kubaki au la.
Urusi, ambayo imekuwa ikiisaidia serikali ya
Rais Assad kwa hali na mali, imepinga madai kwamba Rais Assad anafaa
kuondolewa madarakani.
Lakini baada ya kuzungumza na Waziri wa Mashauri
ya Nchi za Nje wa Marekani, Hillary Clinton, Waziri wa Mambo ya Kigeni
wa Urusi, Sergei Lavrov, alishikilia kwamba kuna matumaini makubwa ya
kupata makubaliano.
Bi Clinton kwa uapnde wake alisema bado kuna tofauti na matatizo baina yao.
No comments:
Post a Comment