Si unafahamu kwamba Dogo Janja alirudi kwao Arusha baada ya kujiondoa
TIP TOP lakini akarudishwa Dar na kundi la WATANASHATI ambalo ndio yuko
nalo sasa hivi?
Sasa stori ni kwamba Baada ya meneja wake wa sasa wa WATANASHATI kusema
kwamba yuko tayari kumuachia Dogo Janja kuchukuliwa na mtu yeyote ambae
ataweza kumuendeleza vizuri kisanii na kimasomo hata TIP TOP wenyewe
kama wakijirekebisha, Janja ameamua kutoa maneno matano kuhusu kurudi
Tip Top kama wakijitokeza kwa hiyo ofa.
Amesema “Mimi kama mimi siko tayari”
Meneja Ostaz Juma alitangaza hiyo ofa juzi exclusive kwenye AMPLIFAYA ya
CLOUDS FM na kusema yeyote atakae taka kumchukua Janja mikononi mwake
itabidi amlipe gharama alizotumia, kauli ambayo iliwashtua wengi japo
mpaka sasa Janja yuko mikononi mwa WATANASHATI.
|
No comments:
Post a Comment