Maji ya AcidPolisi katika kisiwa cha Zanzibar wamesema wanawake wawili wa Uingereza wamerushiwa maji ya Acid katika nyuso zao baada ya kuvamiwa mwendo wa usiku.Naibu kamishna wa polisi amesema kuwa wanaume wawili waliwatendea wanawake hao kitendo hicho walipokuwa wakitembea katika barabara za mji wa kihistoria wa zanzibar.
Amesema kuwa polisi tayari wameanzisha msako dhidi yao wanaume hao.
Wanawake hao, wanasemkana kufanyia kazi shirika moja la kujitolea na nia ya shambulizi hilo haijulikani.Polisi wanasema kuwa wanawake hao wenye umri wa miaka 18 walikuwa wakitembea katika mji wa Mawe kisiwani Zanzibar ambao ni kivutio kikuu cha utalii kisiwani humo, wakati wanaume wawili waliokuwa wamepanda piki piki walipowamwagia Acid kwenye mikono , vifua na nyuso zao.
Wanawake hao wanaoaminiwa kuwa ni wahudumu wa kujitolea wa shirika la misaada, walipelekwa kwa ndege hadi Dar es Salaam ambako wanapata matibabu . Afisa wa wizara ya afya amesema kuwa majeraha yao si ya kutishia maisha .
Polisi wa Zanzibar wamesema ni mara ya kwanza kwa raia wa kigeni kushambuliwa kwa namna hiyo na kwamba wanawasaka wahusika.Zanzibar ni kisiwa kinachokaliwa na idadi kubwa ya waislam na shambulio hilo linakuja katika kipindi cha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan , wakati watu wakisherehekea sherehe za Eid.Kwa hisani ya http://www.matukiodaima.com/x
No comments:
Post a Comment