Polisi nchini Kenya wameelezea BBC kuwa watoto 2i wamekwama nyumbani
kwao baada ya kufukiwa na tope na maji yaliyosababisha maporomoko ya
ardhi.
Watoto
hao walikuwa wamelala katika kijiji cha Narok kilomita kadhaa kutoka
mji wa Nairobi, mvua kubwa iliponyesha na kusababisha maji kusomba
majumba kadhaa katika mtaa wao.
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya limeonya watu wanaoishi
maeneo yanayotishiwa kukumbwa na mafuriko wahamie sehemu za juu na
milima.
Mvua kubwa imekuwa ikinyesha katika sehemu nyingi nchini humo na inaaminiwa kuendelea kunyesha.
Katibu mkuu wa shirika hilo nchini Kenya Abbas
Gulet ameambia BBC kuwa maeneo yaliyoahiriwa zaidi ni pamoja na Nairobi
na maeneo yaliyo pembezoni, na garissa ambapo watu kadhaa wamefukiwa na
maporomoko ya ardhi au kuzingirwa na maji.
Maafa makubwa
Kufikia sasa watu 36 wamefariki kutokana na mafuriko hayo yaliyoanza chini ya mwezi mmoja.
Kawaida msimu wa mvua nchini Kenya huwa kati ya
mwezi Machi na May, lakini wadadisi wanasema kuwa safari hii mvua
imenyesha kwa wingi zaidi.

No comments:
Post a Comment